ELIMU KWA WANANCHI LUDEWA JUU YA SERIKALI ZA MITAA

Waipa lawama serikali kwa kuchelewa kutoa vitendea kazi mapema serikali za mitaa Siku chache zimebaki ili uchaguzi wa serikali za mitaa ufanyike hapa nchini Tanzania ambapo uchaguzi huo unategemea kufanyika Desember 14 mwaka huu 2014 Hivyo baadhi ya wananchi wilayani ludewa katika mkoa wa njombe wamesema bado hawana uelewa wakutosha juu ya uchaguzi huo. ​Viongozi watakao chaguliwa ni kama ilivyoneshwa hapo juu. Wakizungumza na mwanahabari wetu Maeneo ya ludewa Mjini mapema desember 6 mwaka huu wananchi hao ambao ndio wapiga kura walisema kuwa licha ya uchaguzi huo kuwa muhimu lakini bado wao mpaka sasa hawaelewi kwa kina zaidi kwakuwa uchaguzi wa mwaka huu umekuwa na changamoto nyingi ambazo zimesababisha uchaguzi huo kutofanyika kwa kiwango cha asilimia kubwa. Wananchi hao walisema bado wamekuwa na changamoto juu ya kutofautisha daftari la kudumu la wapigakura na kitendo cha kujiandikisha katika daftari la wapigakura la serikali za mitaa hali ambayo itawafanya wananchi wengi washindwe kuwachagua viongozi wanaowataka kutokana na changamoto walizo kutana nazo wakati wa kujiandikisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Hata hivyo waliongeza kuwa kuna wananchi wengi ambao bado hawajajiandikisha katika daftari la kupiga kura kutokana na serikali kuchelewesha vitendea kazi hasa madaftari hayo ikiwemo baadhi yao kuishi katika mazingira ya mbali kutoka ludewa mjini hivyo wananchi hao wakikosa haki yao ya msingi wamesema kuwa makosa hayo yatakuwa ya serikali. Pia walisema mchakato wa kuwapata viongozi wa serikali za mitaa ulikuwa umejaa vitendo ambavyo si sahihi kutoka kwa baadhi ya maeneo hasa Rushwa ikiwemo kuwadanganya wapiga kura katika maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania Huku wakiiomba serikali kusimamia kikamilifu uchaguzi huo ambao unatarajia kufanyika kuanzia Desember 14 mwaka huu.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: