Mastaa wa Bongo Wamejaa Zambi na Kutumia Muda Mwingi Kupiga Majungu.

WAKATI tukiwa tunakaribia kumaliza mwaka 2014, msanii wa filamu Ruth Suka ‘Mainda’, amedai kuwa hakuna jambo ambalo mastaa wa Bongo wamelifanya zaidi ya kuchuma dhambi na kutumia muda mwingi kupigana majungu kuliko kumcha Mungu kwa matendo mema. Akizungumza na gazeti la Uwazi, Mainda alisema kuwa ndani ya tasnia ya filamu bado mambo ni magumu kwani mastaa wengi wamekuwa nyuma na matendo ya Mungu kwa kufanya anasa kila kukicha huku wengine wakizidi kuchafuana kwa kupigana majungu. “Ni kweli mwaka umeisha lakini lazima tujue wapi tumekosea, lakini wasanii wetu hawana roho ya kuamini kuwa Mungu yupo ndiyo maana wanapigana majungu kila kukicha. Tangu kifo cha kipenzi Kanumba kutokea nilisemwa sana na baadhi ya wasanii wakidai kuwa siwezi kuwika tena lakini wanasahau kuwa niko bize na kazi ya Mungu na si kupiga majungu au kukaa kijiweni kumsema mtu,” alisema Mainda.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: