VIONGOZI WA CHADEMA WATEKWA NA MAJAMBAZI HUKO KAHAMA WAKITOKA KWENYE KAMPENI

Msafara wa viongozi na wanachama wa chama Demokrasia na Maendeleo Chadema wa Kanda ya ziwa Magharibi wametekwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wakitoka kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za serikali za Mitaa kata ya Bulyanhulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Akizungumza na waandishi wa habari ikiwemo Malunde1 blog, Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kahama, Juma Protas(PICHANI)alisema tukio hilo lilitokea juzi katikati ya Kijiji cha Kalagwe kata ya Ntobo na Kijiji cha Nyambula Kata ya Ngongwa majira ya Saa 3:30 Usiku wakati wakitoka kwenye Kampeni Kijiji cha Kakola. Akizungumzia tukio hilo Protas alisema walipofika eneo la Daraja walikuta magari matatu yamesimama pembeni ambayo ni Basi la Jordan ambalo lilikuwa linatoka mkoani Geita kuelekea Kahama,Roli aina ya Fuso na Gari ndogo inayomilikiwa na Kampuni ya TBL kupitia bia ya Balimi ambayo nayo yalikuwa yametekwa. Alisema wakati wanajaribu kuyapita magari hayo ghafla waliona Mawe na Miti ambayo ilikuwa imetandazwa barabarani na ndipo majambazi hao waliamuru Msafara huo ambao ulikuwa na magari mawili wenye watu 10 wasimame na watoe simu na fedha walizokuwa nazo. “Tulisikia sauti wakisema zimeni taa za gari na muziki na hatuwezi kuwadhuru nyinyi Makamanda ila tunataka fedha na simu, na tupo kazini mnatakiwa kuwalaumu viongozi waliokula Pesa za Escrow bila hiyo tusingefanya haya mnayoyaona”alifafanua Protas. Aliwataja waliokuwemo kwenye msafara huo kuwa ni mratibu wa Kanda ya ziwa mashariki Renatus Mzemo, Mwenyekiti wa Kamati ya Rasilimali Kanda ya ziwa Magharibi, Emmanuel Mbise na Mwenyekiti wa Kamati ya Uenezi wa chama hicho Kanda hiyo Juma Protas ambaye ndiye Mwenyeki wa Chadema. Viongozi hao wa Chadema walikuwa wamepanda gari aina ya Toyota Prado yenye no. T 707 BBP ambayo hata hivyo ilivunjwa baadhi ya vioo. “Tuliibiwa fedha tathimini zaidi ya shilingi laki tisa pamoja na simu 11 ambazo hazikufahamika mara moja thamani yake na gari yetu moja ambayo ni ya mdau alyejitolea kutusaidia ilivunjwa vioo na ile ya M4C yenyewe walisema hawawezi kuivunja maana ni wananchi walichanga kuinunua”,aliongeza Protas “Kulikuwa na magari mengi tuliyoyakuta yametekwa na abiria walinyang’anywa simu na fedha zao, pia kulikuwa na Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Lunguya ambaye alitekwa akiwa na pikipiki na wakamfunga Kwenye mti pamoja na ddugu yake na baada ya kuchukua fedha walitoweka kusikujulikana”,AliongozeaMwenyekiti huyo. Hata hivyo Jeshi la Polisi wilayani Kahama lilifika eneo hilo baada ya kupewa taarifa na abiria waliokuwa kwenye basi ambalo lilitekwa na kukuta majambazi hayo yakiwa yametokomea kusikojulikana na kutoa msaada wa kiusalama kwa magari yote na abiria waliotekwa. Na Ndalike Sonda-Malunde1 blog Kahama @mulembe
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: