WILAYA LUDEWA MKOA WA NJOMBE NA CHANGAMOTO YA HUDUMA YA AFYA

Kutokana na changamoto ya ukosefu wa huduma ya afya hasa matibabu katika kijiji cha masimavalafu kilichopo katika kata ya ibumi wilaya ya ludewa mkoa wa njombe wananchi wa kijiji hicho wameamua kujiunga na kuwa kitu kimoja kwa kuanzisha ujenzi wa jengo la zahanati katika kijiji hicho. Akizungumza na Redio best fm Diwani wa kata ya Ibumi kwatiketi ya chama cha mapinduzi ccm mh Edward Haule alisema kuwa wananchi hao wameonesha hali ya umoja na mshikamano kwa kuamua kujitolea na kuanzisha ujenzi huo wa zahanati ya kijiji chao ujenzi ambao ulianza rasmi mwezi September mwaka huu 2014. Aliongeza kuwa kwasasa ujenzi huo umeanza kwa ngazi ya kukamilisha msingi wa mawe kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na viongozi wao wa kata na kijiji kwalengo la kuwasaidia wananchi hao kupata huduma ya matibabu ndani ya kijiji chao cha masimavalafu. Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wamewashukuru viongozi wa kata ya ibumi na wilaya ya ludewa kwa kushirikiana na wananchi hao kutokana na changamoto waliyokuwawakikutana nayo wananchi hao yakutembea umbali mrefu kufuata huduma ya matibabu na kusababisha kusafirisha wagonjwa kuelekea ibumi kwa kutumia muda mrefu zaidi. Walisema kijiji chao kimekuwa mbali na makao makuu ya kata ya ibumi hivyo huduma nyingi wamekuwa wakizifuata ibumi licha ya kuwa ni mbali hasa suala zima la matibabu kwakuwa kijiji hicho mpaka sasa hakina zahanati ambayo inatoa huduma ya afya kwa wananchi. Hata hivyo wananchi hao wanawaomba wadau na wafadhili mbalimbali hapa nchini tanzania kuwasaidia na kujitolea michango yao ili kufanikisha kazi ya ujenzi wa jengo hilo la zahanati ya kijiji cha masimavalafu katika kata ya ibumi wilaya ya ludewa mkoani njombe.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: