KALI YA MWAKA....MTOTO WA MIEZI 3 ABAINIKA KUWA MWATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA HUKO DAR

Mtoto mwenye umri wa miezi mitatu mkazi wa Buza,Dar es salaam amebainika kuwa mwathirika wa dawa za kulevya. Damu na mkojo vya mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa vilichukuliwa na kupimwa katika Maabara ya hospitali ya Mwananyamala na baada ya saa mbili majibu yalitoka yakionyesha kuwa alikua na chembechembe za dawaza kulevya aina ya Heroine. Taarifa za kitabibu ziaonyesha Heroini katika mwili wa binadamu huweza kuonekana katika mkojo ndani ya siku mbili hadi nne endapo dawa hizo zilitumika na muhusika kwa kati ya saa mbili hadi tano. Mtaalamu wa tibawa hospitali hiyo Elifasi Mritu anasema ‘Ni kweli ukitumia dawa hizo wakati wa kunyoshesha ama ukiwa na mimba mtoto naye huathirika’. Mama wa mtoto huyo Zena au maarufu kama Zerish alisema alipata ujauzito wakati akitumia dawa hizo za kulevya hadi sasa na anapovuta ama kujichoma mtoto wake pia hupata ‘stimu’kwa sababu hupata dawa hizo kupitia maziwa anayonyonya na hivyo wote wawili kulala fofofo sehemu yoyote.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: