POLISI WATUMIA MABOMU NA RISASI ZA MOTO KUSAMBARATISHA WAENDESHA BODABODA HUKO GEITA
Jeshi la polisi Mkoani Geita limelazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya waendesha pikipiki (BODABODA), baada ya kuzingira nyumba ya mfanyabiashara anayesadikiwa kuwa ni mwizi wa pikipiki na kutaka kuichoma moto.
Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya mashuhuda wameimbia blog hii kuwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Joseph (36) mkazi wa Msalala Road, akiwa amembeba abiria wake Saada Nasorwa (37), walizingirwa na waendesha pikipiki wakitaka kuwachoma moto.
Tukio hilo limetokea jana saa mbili asubuhi, katika maeneo ya NMB Bank ambapo watu hao walikuwa wanaendesha pikipiki yao yenye namba T 234 AVH aina ya sanlg kuelekea makao makuu ya polisi Mkoa.
“Sisi tumewaona watu hawa wakipita hapa wakiwa wamebebana lakini muda mfupi baadaye tuliona waendesha bodaboda wakiwafukuzia huku wakisema ni wezi, wakamatwe, wachomwe moto, wametuchosha kutuibia pikipiki na kuwaua wenzetu,”walisema mashuhuda hao.
Inaelezwa kuwa mfanyabiashara huyo Juma amekuwa akiwatumia vijanakupanga njama mbalimbali za kuiba pikipiki na wakati mwingine kutekeleza mauaji kwa waendesha bodaboda jambo ambalo limekuwa ni kero kwa wananchi wa Mkoa wa Geita.
“Taarifa nyingi za huyu jamaa ziko polisi lakini tunashangaa kila akikamatwa anaachiwa huru na kurudi uraiani na kutusumbua sisi wananchi kwanini asifungwe? Na wakati ushahidi tunapeleka yeye ni nani?”alihoji Masanja ambaye ni mwendesha bodaboda.
0 comments:
Post a Comment