JANGILI WA KIMATAIFA AKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM

Polisi wa kimataifa , interpol tawi la Tanzania wamemkamata mfanyabiashara maarufu raia wa Kenya kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili pamoja na uhalifu uliovuka mipaka ikiwemo mauaji ya tembo . Mtuhumiwa huyo Mohamed Ally Feisal amekamatwa mjini Dar-Es-Salaam baada ya kusakwa kwa kipindi kirefu kwa makosa hayo ya kimataifa. Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Bwana Diwani Athumani kutoka kamisheni ya Kurugenzi ya makosa ya jinai amesema mtuhumiwa huyo anakabiliwa na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kimataifa ikiwemo uwindaji uliovuka mipaka kimataifa katika nchi mbali mbali. Bwana Athumani Diwani alieleza kuwa kwa sasa mtuhumiwa huyo anashikiliwa huku upelelezi ukiendelea kujua makosa mengine aliyoyafanya kuhusiana na biashara za bidhaa zitokanazo na Tembo ndani ya Tanzania na katika nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo nchi yake ya Kenya. Mohamed Feisal Ally amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za uwindaji haramu husani mauaji ya Tembo tatizo ambalo ni kubwa hususani katika ukanda huu wa Afrika Mashariki hasa Kenya na Tanzania ambapo idadi kubwa ya Tembo wamekuwa wakiuawa kila mwaka na kutishia kutoweka kwa viumbe hao
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: