HIVI NDIVYO MAXIMO NA MSAIDIZI WAKE WALIVYOTIMULIWA KUINOA KLABU YA YANGA

Klabu ya Yanga na wawakilishi wa michuano ya shirikisho ya Afrika imewatupia virago rasmi makocha wabrazil Marcio Maximo na msaidizi wake, Leonardo Neiva kwa kile kinachoelezwa kutofurahishwa na mwenendo wa timu katika ligi licha ya kuwa na wachezaji wengi mastaa wa kigeni na kutumia mamilioni katika kusajili wachezaji mahiri wa kigeni. Yanga hivi karibuni ilimsajili mrundi na mfungaji bora msumu uliopita, Hamis Tambwe kutoka kwa mahasimu wao (Simba) akiungana na Mliberia, Kpah Sherman, Wanyarwanda Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Mbrazil Andrey Coutinho kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni Tayari uongozi wa Yanga, katika kile kinachoonekana pesa si tatizo, chini ya Mwenyekiti bilionea Yusuf Manji umemrudisha klabuni aliyekuwa kocha wa zamani, Mholanzi Van de Pluijm, atakayesaidiwa na kocha mzalendo na mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa na klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa. Katika maelezo yake, Manji amewatakia kila la kheri wabrazil hao na kusema na mungu akipenda wataendelea kushirikiana nao katika siku za usoni. Tayari makocha hao wawili , Pluijm na Mkwasa wameshatambulishwa kwa wachezaji wa Yanga na habari za uhakika kutoka klabu hapo zinasema baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu, Pluijm, aliyewahi kuipatia yanga mafanikio katika ligi kuu, ana anza kibarua chake rasmi leo. Hata hivyo, kuondoka kwa Maximo, aliyewahi kuajiriwa na Serikali ya Tanzania kama kocha mkuu wa timu ya taifa, Stars Stars katika miaka ya nyuma na kurudi nchini kivingine kuongoza Yanga
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: