FORUM CC YAWASILISHA MAPENDEKEZO KWA WAZIRI MAHENGE

Forum CC leo imewasilisha mapendekezo yao kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais mazingira Binilith Mahenge kuelekea mkutano wa Kimataifa wa Tabia Nchi. Ujumbe huo wa Forum CC ukiongozwa na Meneja mwezeshaji wake Rebeca Muna umepeleka mapendekezo hayo na kumkabidhi Waziri mwenye anayehusika na Mazingira ambapo umebainisha kuwa serikali inapaswa kubainisha mapendekezo ya kupunguza makali ya uharibifu wa mazingira nchini. Kuhusu nchi zilizoendelea ujumbe huo umezitaka zikubali kuwepo na makubaliano ya kisheria na kuheshimu kanuni juu ya masuala yote ya mazingira ya duniani.Nchi hizo zimetakiwa pia kutoa fedha ,teknolojia na kujenga uwezo juu ya kukabiliana na janga la uharibifu wa mazingira. Katika hatua nyingine ujumbe huo umetoa rai kwa viongozi wa dunia na Afrika kuwashirikisha wadau wengine katika mchakato wa mikataba ya kimataifa ili kupunguza manung’uniko ya kutoshirikishwa kwa wadau katika masuala yanayohusu mazingira.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: