SUMATRA: ATAKAYEPANDISHA NAULI MSIMU WA CHRISTMAS ‘KUKIONA

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) limewataka Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) kufuata sheria na masharti ya leseni zao kwa kutoza nauli kama ilivyoidhinishwa na Baraza hilo kuelekea sikukuu za Krismas na Mwaka mpya. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dokta Oscar Kikoyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Katika mkutano huo amesema kuwa kutokana na wingi wa abaria kipindi cha sikukuuu mahitaji ya usafiri huwa makubwa kulingana na huduma zilizopo hivyo watoa huduma huchukua fursa hiyo kuongeza kiwango cha nauli na wengine kulangua tiketi kinyume na masharti ya laseni zao. Ameongeza kuwa wamiliki wa Mabasi wanatakiwa kuwa makini na wafanyakazi wao kutojihusisha na vitendo vya namna hiyo kwani ikingundulika tiketi za kampuni husika zinalanguliwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa. Katika hatua nyingine Baraza hilo limewataka abiria kutonunua tiketi za safari zao kutoka kwa wapiga debe au vishoka na kutokata tiketi mapema ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanasafiri kwa tiketi zenye majina yao na kiwango cha nauli walicholipa ili kuboresha huduma za usafiri kwa kuzingatia nauli halali zilizopangwa na SUMATRA
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: