EXCLUSIVE: MVUA YAVUNJA PAMBANO LA MTIBWA SUGAR VS STAND, KUCHEZWA KESHO ASUBUHI

Pambano la Ligi Kuu Bara kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Stand United, limeahirishwa. Pambano hilo limeaahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mjini Turiani na kusababisha Uwanja wa Manungu kujaa maji. MTIBWA SUGAR. Awali pambano hilo lilisimama kwa dakika 15, lakini kamisaa Bile Mwilima alipoona alama za uwanja zimefutika, pamoja na utelezi kuwa wa hali ya juu, akatangaza kuliahirisha. Kutokana na hali hiyo, pambano hilo ambalo hadi linavunjika lilikuwa sare ya bila mabao, litachezwa kesho saa mbili asubuhi. Kwa mujibu wa kamisaa huyo pambano hilo litachezwa kesho kuanzia dakika ya 6. @salehe jembe
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: