Baada ya Mr. Flavour kukataa kuingia kwenye ndoa, staa huyu mwingine naye ana msimamo huu…

Jivunie kuwa mwana ludewa


Timaya2
Mr. Flavour alisema hayuko tayari kuoa kwa sasa kwa sababu muziki wake bado unamdai, leo kuna staa mwingine ambaye umri wake ni miaka 37 mpaka sasa lakini amesema kuwa hayuko tayari kujivika jukumu la ndoa kwa sasa.

Mkali ambaye wengi tulimfahamu kupitia ile kolabo aliyopewa na P Square, hit-song ya Good or Bad, anaitwa Enetimi Alfred Odom a.k.a Timaya ametoa ya kwake kwamba kwanini hawezi kuingia kwenye ndoa kwa sasa.
… Siko tayari kuoa kwa sasa na kama kuna yoyote anatarajia hilo sio kweli kwa sababu umri wangu bado ni mdogo… Ndoa haiangalii pesa na hakuna yeyote anayejua nina akiba kiasi gani benki kwa sababu wao sio wahasibu wangu… Wanamuziki ni waongo sana, msiamini kila wanachowaambia…“– Timaya.
… Siko tayari kuoa kwa sababu siko tayari kujitoa sadaka kwa mwanamke yoyote… Samahani, mwanangu wa kike ni kila kitu kwenye maisha yangu, ninampenda na suala la ndoa halipo kichwani kwangu hata kidogo… Sihitaji kujikuta kwenye hali kwamba namuaga mwanamke kwamba ninaenda safari halafu anaanza kunilalamikia...”– Timaya.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: