Amanda: Starehe Kwanza, Mungu Baadaye.

Staa mwenye shepu ya aina yake ndani ya Bongo Movies, Tamrina Poshi ‘Amanda’ ameibuka na kusema kuwa siku ikifika atarejea kwa Mwenyezi Mungu lakini kwa sasa bado anakula ujana. Akiongea na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Amanda alisema kwa sasa umri wake unamruhusu kula ujana kwa mambo ya starehe kama kuvaa mavazi ya kuacha mwili wake nusu utupu kwa sababu muda wa kurejea kwa Mungu bado haujafika. “Jamani niacheni na mavazi yangu, ukifika muda nitarejea naona mnanisema sana, kama wewe Mungu amekujalia kusali, mshukuru mimi muda huo bado haujafika,” alisema Amanda ambaye wakati huo alikuwa ametupia kivazi kilichomuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake hasa tumboni.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: