SAKATA LA ESCROW: MUHONGO AJITOA MUHANGA KUOKOA JAHAZI

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospete Muhongo ameikingia kifua serikali kuhusiana na wizi wa zaidi ya Bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kutokana na kuwepo mgogoro baina ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL na Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco). Waziri Muhongo ameanza kwa kutoa pongezi juu ya mjadala wa Escrow ambapo amesisitiza kuwa mengi yamesemwa na ni wakati wa kuanza mjadala kujua ukweli wa sakata hilo. Kuhusu Escrow Muhongo amesema Account ya Escrow ilipaswa kuwa na bilioni 306 zilizowekwa na TANESCO fedha ambazo Waziri huyo amesema sio za umma. Taarifa hiyo inakinzana na ripoti ya PAC iliyothibitisha kuwa ni fedha za umma na mchakato wa kutoa pesa Escrow umegubikwa na mchezo mchafu ikihusisha kutakatishwa fedha na benki mbili nchi. Madai kwamba IPTL inaidai IPTL 321 Bilioni, amesema kwamba bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai haya na vitabu vya TANESCO vinavyokaguliwa na CAG hakionyeshi madai haya. Amesisitiza kwamba TANESCO kwa kushirikiana na IPTL ilifanya uhakiki ili kujua madai halali ya IPTL kabla ya kufanya malipo. Deni la TANESCO kama capacity charge lilikuwa $370milioni ambazo ni pungufu ya $90 milioni ya madai ya IPTL. Yalifanyika hoteli ya Kunduchi na majina ya waliokuwepo anawataja. ” Hizi takwimu zinaonyesha hakuna fedha yetu pale tunayodai bali tunadaiwa na IPTL. Hamna fedha ya umma popote bali tunadaiwa na makampuni ya uzalishaji umeme(anataja makampuni na madeni wanayodai “. A lisema Muhongo Kuhusu mjadala uliokuweo kama fedha za Escrow ni mali ya umma au ni TANESCO Prof. Muhongo amesema kwamba Hakuna fedha ya umma katika akaunti ya Escrow fedha zote ni mali ya kampuni ya IPTL. Katika hali isiyokuwa ya kawaida utetezi huo wa Waziri wa Nishati na Madini hadi Bunge linamaliza kikao wabunge hawakuweza kugagiwa ripoti hiyo licha ya kuiomba kwa nguvu huku wakipiga kelele kabla ya Waziri huyo kukamilisha ripoti yake
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: