SAKATA LA ESCROW: KILA MTU AFE NA MSALABA WAKE KUTIMIA LEO
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Abdulrahman Kinana katika moja ya vikao vyake alibainisha kwamba wanaohusika na sakata la upotevu wa Bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa inatunza fedha za mgogoro kati ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL pamoja na shirika la Umeme Tanzania(TANESCO). Je, msemo wa kila mtu uliotolewa na Bw. Kinana kutimia leo?
Ripoti ya Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali iliyowasilishwa jana imewataja baadhi ya vigogo wanaohusika na kashfa ya IPTL Nchini Tanzania akiwemo Waziri Mkuu na kuwataka kuwajibika kisiasa na kisheria. Kamati hiyo imewataja viongozi wengine wanaotakiwa kuwajibika kutokana na kashfa hiyo kuwa ni mwanasheria, Waziri wa nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati pamoja na viongozi wengine wa bodi.
Katika ripoti hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe na makamu mwenyekiti wake Deo Filikunjombe, imethibitisha kuwepo mazingira ya udanganyifu na ufisadi katika mchakato wa malipo yaliyofanyika na kueleza kuwa upotevu huo wa fedha ungeweza kudhibitiwa kama kungekuwa na uwajibikaji wa kutosha kwa baadhi ya viongozi.
Katika hatua nyingine, wananchi wanasubiri kwa hamu kubwa kujua nini kitatokea kufuatia waliotajwa kuiba fedha hizo kuwa ni Viongozi wakubwa serikalini kama Mawaziri pamoja na watendaji wa wengine wa kisiasa na viongozi wa dini.
0 comments:
Post a Comment