MTOTO MWENYE ULEMAVU ABAKWA NA KUAMBUKIZWA MAGONJWA YA NGONO HUKO MBEYA

Mtoto mlemavu wa akili na miguu mwenye miaka14 anadaiwa kubakwa na kuambukizwa magonjwa ya zinaa na mwanaume mwenye umri wa miaka50. Mwanaume huyo anadaiwa kufanya kitendo hicho siku moja kabla ya kufunga ndoa na mke mpya aliyemlipia mahari eneo la Uyole Mbeya baada ya kuachana na mke wake wa kwanza aliyezaa naye watoto zaidi ya watatu. Tukio hilo lilitokea November 4 na kuripotiwa kituo cha polisi ambapo mpaka sasa mtuhumiwa anasakwa na polisi kwa ajili ya ufunguliwa kesi ya kubaka. Shangazi wa mtoto huyo akizungumza kwa masikitiko alisema waligundua mtoto wao amefanyiwa kitendo hicho baada ya kutoka kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo huku akilia na walipomchunguza ndipo walipobaini kuwa amebakwa na vipimo vilionyesha ameambukizwa magonjwa ya zinaa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: