Rais Mstaafu na sera ya kilimo kwanza

Wakati wa utawala wake Rais Ali Hassan Mwinyi alitembelea mikoa mbalimbali kuhimiza shughuli za kilimo. Katika ziara yake aliwakosha sana wananchi wa mkoa fulani baada ya kutumia lugha tata. Mheshimiwa sana alisema hivi..."Ndugu zangu kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu, lakini kwa vile watu wengi wadhani kichwa ndio cha maana kuliko mgongo basi wafanya dharau. Mie leo nimekuja kuwahimiza ndugu zangu ili mkazane kwenye mashamba yenu. Nyie ndugu zangu wa Songea kazaneni kwenye mahindi tena kazaneni haswa! na ndugu zangu wa Bukoma kazaneni kwenye migomba na mikorosho, tena mkazane kweli kweli. Na mlioko Tunduru kazaneni kwenye mikorosho maana hilo ndio zao lenu la biashara hivyo msione aibu hata kidogo kazaneni kwelikweli...." Mheshimiwa alishangaa na kusita kuendelea kuzungumza baada ya kuona wananchi wakishangilia kwa makofi na nderemo nyingi huku wengine wakivunjika mbavu kwa kucheka.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: