Hata Rais yalimchanganya...

Miaka michache iliyopita Rais Ali Hassan Mwinyi (wakati huo) alifanya ziara ya kiserikali Songea (Mkoa wa Ruvuma) kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo vijijini. Mara tu baada ya mapokezi, mkuu wa mkoa huo (Jina kapuni) alimsomea Rais Mwinyi ratiba ya siku hiyo kama ifuatavyo: "Mheshimiwa Rais wananchi wa mkoa wa Ruvuma wanakukaribisha kwa moyo mkunjufu na wako tayari kukuonesha maendeleo waliyofikia katika shughuli mbalimbali. Hivyo ili kuweza kukidhi kiu ya wananchi wa mkoa huu, tumepanga kwamba kesho asubuhi chai utakunywa na kapanya, chakula cha mchana utakula na nguruwe halafu utalala na mtumbo" Rais (Alhaji) Ali Hassan Mwinyi akasema "Astaghafirulahi, futeni hiyo ratiba mie siwezi hayo mambo mlonipangia...ati nile na nguruwe? Mkuu wa mkoa akamwambia "Mheshimiwa Rais utuwie radhi, hayo ni majina ya vijiji vyetu Nakapanya, Nanguruwe na Namtumbo..." Mwinyi akavunjika mbavu kwa kicheko...
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: