news alert: SPIKA ASITISHA BUNGE HADI WATAPOJADILIANA TENA BAADA YA SINTOFAHAMU WAKATI WA MJADALA MKALI WA SAKATA LA ESCROW

Sintofahamu iliyotokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma Ijumaa Novemba 28, 2014 imepelekea Spika Anne Makinda (pichani) kulazimika kusitisha shughuli za Bunge mpaka hapo watapojadiliana tena. Hii ni baada ya majadiliano makali kuhusu kuwajibishwa ama la kwa viongozi wanaohusika na sakata la akaunti ya Escrow. Hali hii iliibuka baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA na kambi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe kuinuka na kusema kuwaBunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, na kwamba kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kutoka maamuzi kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. "Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi", alisema Mhe. Mbowe.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: