GHANA YATUPWA NJE MICHUANO YA AFRIKA

Timu ya Taifa ya Ghana ya mpira wa migu chini ya umri wa miaka 17 imeondolewa kwenye michuano ya vijana ya Afrika hapo mwakani baada ya rufaa yake kutupiliwa mbali na CAF. CAF iliiondoa Ghana katika michuano hiyo kufatia kumchezesha mchezaji aliyezidi umri Issac Twumkatika mchezo wa hatua ya raundi ya kwanza walipokutana na Cameroon ambapo Ghana ilishinda kwa bao 2-1 mchezo wa kwanza na mchezo wa pili ikashinda 4-3. Lakini Cameroon ilipinga matokeo hayo na hivyobasi Shirikisho la CAF likaamua kumpiga marufuku Twum. Shirikisho hilo lilifichua kuwa mchezaji huyo ambaye aliwahi kuiwakilisha timu yake ya vijana ya Kpando Heart Lions nahivyo alifeli mahitaji ya kushiriki katika mechi hizo baada ya kufanyiwa ukaguzi wa miaka yake. Rufaa huenda ikawasilishwa dhidi ya uamuzi huo wa CAF katika mahakama ya usuluhishaji wa migogoro ya michezo katika kipindi cha siku 10 zijazo. Kamati kuu ya shrikisho la soka nchini Ghana inakutana hii leo ili kutafuta hatua watakayochukua.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: