MWANDOSYA: ‘ SAKATA LA ESCROW LIMEISHUSHA HADHI TANZANIA

BUNGENI, Mbunge wa jimbo la Rungwe ambaye pia ni Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais- Asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mark James Mwandosya amesema kwamba sakata la Escrow limeishusha hadhi ya Tanzania mbele ya Wananchi ndani na nje ya nchi. Hatua hiyo pia imeonekana wazi kufuatia baadhi ya wahisani kusitisha kutoa misaada hadi pale hatua kali zitakapochukuliwa dhidi ya wanaohusika na sakata hilo Akitoa hoja Bungeni leo Prof. Mwandosya amelitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lichukue maamuzi magumu ili haki itendeke na kuweza kurudisha imani kwa watanzania inayoonekana kupotea hivi sasa. Ameongeza kuwa serikali inatakiwa kuangalia mapungufu yaliyotokea hadi kupelekea fedha ya umma inaibwa katika Benki kuu ya Tanzania. Kutokana na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Muhongo kupinga kwamba fedha zilizokuwemo katika akounti ya Escrow sio za fedha za umma Mbunge huyo amesisitiza kwamba fedha yeyote iliyopo Benki kuu ni fedha ya umma, hivyo basi hiyo fedha ni dhahiri kuwa ni umma. Katika hatua nyingine amewataka wabunge kuwa na imani na kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali kutokana na kuwepo wabunge wengi kutoka ndani ya kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge Zitto Kabwe
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: