MADEREVA BAJAJI WAINGIA MJINI, WAPIGA KAZI MBELE YA POLISI
Sheria ya kupiga marufuku vyombo vya usafiri wa kubeba abiria maarufu kama Bajaji na Boda boda huenda ikawa imeisha nguvu. Hatua hiyo inafuatia baadhi ya madereva bajaji na Boda boda kuingia katikati ya mji (CBD) na kuendelea na michakato ya kushusha na kupakia abiria mbele ya askari wa usalama barabarani.
Akizungumza na Mwandishi wetu wa Habari mmoja wa Madereva Bajaji ( jina linahifdhiwa) amesema kwamba wameamua kuingia katikati ya mji katika eneo la Posta jijini Dar es salaam kufanya kazi kutokana na kuwa na abiria wengi na wanaolipa vizuri ukilinganisha na abiria waliopo katika maeneo mengine.
Alipoulizwa kuhusu kama watanatoa rushwa ili waweze kufanya kazi katika maeneo yaliyokatazwa amesema kwamba ni kweli wana wawezesha baadhi ya Askari Polisi ili waweze kufanya kazi kwa uhuru.
Katika hatua nyingine, Kamanda wa Kanda maalumu ya Dares salaam Suleiman Kova hivi karibuni amesisitiza kwamba bado sheria ya kukataza Bajaji na Bodaboda kutoingia mjini inafanya kazi na yeyote atakayekamatwa atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kutozwa faini
0 comments:
Post a Comment