DEREVA TOYO sehemu ya 10a

Ilipoishia Jana "ayaaaaa mzeee basi mzeee utaniumiza huku mzee" "wewe baba jimi usimpige huko bwana wewe" "wacha nimpige huko huko maana toka aanze hio toyo yake amekua mtu wa wanawake kila siku huyu....maana juzi nilimkuta kasimama na mwanamke mkubwa kuliko hata wewe mama ake?" "haaaaaaa unasemaje baba jimi?" "ndio hivyo" "mungu wangu we mtoto sijui nikupige wapi we mwana haramu mkubwa wewe" Sasa mama alipandisha mori kuskia nilikutwa na jimama kuliko yeye... Mara mama kanyanyua panga lile la mzeee... linawaka waka kwa ukali wake..... "heeee we mama jemsi panga la nini tena?" ENDELEAAA Mzee ndio alimuuliza mama Kwa vile alivyoshika panga lile. "nataka nimtoe alama huyu mtoto" "ah ah sikiliza mke wangu.... hizo hasira ni za bure tu... kwani ukishamtoa hio alama unayotaka kumtoa.. basi hio mihasira yako ikiisha utajutia jambo hilo" "baba jemsi niache" "aaisee mama jimi kwa hili siachi ng'oo" "kwaio unamtetea kwa ujinga alionao?" "ujinga gani wewe mwanamke?" "si huko kutembea na watu wazima" "basi tufanye nilikudanganya" Mama alikua anatetemeka mikono balaa.. mpaka nikajua leo chululuu yangu inakatwa, Ila baba ni baba tu ndani ya nyumba, kwani alilisovu lile tatizo lakini mama kaganda kwenye jambo moja tu la kuoa... Yaani hawa wazazi sijui wananitafutia nini aisee duuu.... Basi mtoto wa kiume nilitoka pale na kuelekea zangu kijiweni maana ni kama unavyojua kua sasa hivi tayari nimeshakua dereva toyo... kwani yule mzee alishinipa toyo yake nipigie kazi huku nikisubiri ya mjomba ije, Nilifika kijiweni kama kawaida ya kubeba abiria kwa zamu... basi nilikua nmetulia zangu huku nikiskilizia maumivu ya kipigo nilichopewa muda mfupi uliopita, Daahhh tena nilikula mangumi kutoka kwa mdingi duuu ni shidaa... na hapa simuambii mtu ng'oo maana watanicheka kua... mkubwa hivi nimepigwa kama mtoto... Mara mteja alikuja pale anataka toyo kuelekea mjini "oyaaa ni zamu ya juma sasa" Aliongea mmoja wa madereva wenzetu Mara mteja nae akaanza mashauzi maana alikua ni wakike afu ni mzuri huyo aaaa "ah ah jamani mi nataka toyo mpya" Watu wakaangalia toyo zao ikakutwa yangu ndio mpya peke yake maana si nimeanza juzi juzi tu.. "sasa dada hapa sisi tunaenda kwa zamu na istoshe huyu mwenzetu ndio karudi sasa hivi na mteje... sasa itakuaje akubebe na wewe" Ni mmoja wa madereva ndio aliongea hivyo, Na huyu dada akamjibu "kwahio mimi ndio nachaguaa au nyie ndio mnichagulie?" "wewe ndio uchague ila ukumbuke kua na sisi tunatafuta rizki dada angu" Sasa wakiendelea kubishana baina ya dereva toyo mmoja na huyo dada, Mara simu yangu iliita. Niliitoa mfukoni kisha nikaangalia namba na kuikuta ni namba ngeni... Niliipokea na kumsikiliza ni nani anaepiga "Hallo?... nani mwenzangu?" "ni mimi mama roda" "mmhh sikujui mama labda umekosea namba" "hapana ni wewe ndio nimekulenga kukupigia" "mmhh ok sema ulikua unahitaji nini? Toyo au?" "hapana sitaki toyo bali nataka uje unipige picha" "namba zangu ulitoa wapi?" Nilipomuuliza hivyo alishikwa na kigugumizi cha kuongea "Eeh? nii ni hehehehehe nilipata kwenye picha moja hivi ambazo hata mimi nilikuepo" "ulikuepo wapi?" "si pale gaden rose" "aaaaaaa ile sherehe ya kama wiki tatu hivi zimepita?" "ndio" "ok wewe ulivaa nguo gani siku ile?" "bwana njoo utaniona huku huku" "ok nikukute wapi?" "njooo kona ya nairobi utanikuta maeneo ya msikiti pale" "ok poa naja sasa hivi" Niliwasha toyo na kutaka kuondoka. Mara yule dada kumbe alikua anataka nimpakie mimi na wala sio toyo mpya..... "we kaka niwaishe mjini basi" "aaaaAisee dada mi sifiki mjini dada angu" Mara mmoja wa madereva akaropoka kitu "we jemsi? beba likiporo lako.... mteja gani akija anamlenga mtu?.... afu we chaliii kijiweni kwetu hatukutaki...maana kila mwanamke akija ni wewe tuuu... sasa sisi tunakusindikiza au?" "lakini broo? kwani mimi pia si nimetoa mchango wa kijiwe broo?" "hata kama..na kama ni pesa yako tutakurudishia bwana ng'oja tuitafute siku mbili hizi... Au sio madereva wenzangu?" Wakaitikia kwa pamoja na kwa sauti "ndioooo hatumtakiii" Nilijiskia vibaya sema sasa nitafanyaje? maana wao ndio walianzisha kijiwe... Niliongea neno moja tu... kisha nikaondoka na yule dada... mchagua toyo "sawa nitaondoka ila ni mpaka munirudishie pesa yangu" Kisha nikawasha toyo na kuondoka zangu na mteja nikiwa nae..... Nilikua nikilalamika kua nikifukuzwa kwenye kijiwe..!! je nitapata wapi kijiwe kinacholipa vizuri kama hiki.... tena ni kizuri tu na pesa ipo... maana toka niingie hapa kijiweni Yaani wale wanawake masista duu wale wasafi wasafi wote walikua wakija wanataka niwabebe mimi.... sasa ndio maana wananichukia kiasi hiki.... Sasa tukiwa njiani huyu dada alijua sipo katika mudi nzuri ya kikazi leo.. "we mkaka kua makini na mawazo hayo.. kwani tupo barabarani hapa" "usijali dada hapa hadondoki mtu" "lakini mbona wenzako wanakuchukia vile?" "Aaaahh Eti kisa nabeba sana abiria" "mmmh hapana bwana labda kuna lingine" itaendelea,,,,
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: