dereva toyo b
"aaaahhh Sawa nitajaribu kufanya hivyo"
"Eeehh maana mimi mwenyewe sitopanda kwenye toyo zao"
"kwanini sasa?"
"tatizo wananuka vikwapa"
"heee Vikwapa??? toobaaa"
"yaani katika watu wasafi wasafi kidogo kwa hawa madereva toyo ni wachache mno... na mmoja wapo ni wewe"
"mmhhh asante kwa sifa zako"
Sasa kutokana na kupiga stori nikajikuta nimepitiliza mpaka mjini... maana kijiwe chetu kipo pale sombetini kuelekea ngusero.... sasa niliambiwa na mama roda nimkute kona ya nairobi..... sasa nimejikuta nimefika hadi shopraiti...
"we mdada umeona story zako hadi nimepitiliza ee?"
"kwani we ulikua unaishia wapi?"
"si pale kona ya nairobi"
"ok basi mi naishia tu hapo mbele"
Nikaona bora nimfikishe tu maana kama ni kazi nimeitiwa basi huenda nikaikosa
"ni wapi?"
"pale kwenye ile gesti pale"
"gesti tena? Duuu"
"sasa unashangaa nini?"
"mmhh walaaa ila najua kuna jamaa anaenda kujilia vyake huko
"afu wewe mi staki utani wako huo"
"kwani ni siriii?"
"ok ni shing ngapi?"
"buku mbili tu"
"ok chukua kapige maziwa basi"
"daaahh poa sana mdada"
"poaa"
Daahh nilipewa shilingi elfu tano badala ya ya elfu mbili.... Basi mtoto wa kiume niligeuza toyo na kuelekea kona ya nairobi.... kisha nikampigia simu huyo mama roda
"haloo Ee uko wapi? kwani nimeshafika hapa chini ya mti"
"ok mi nipo nyuma yako"
"kwa wapi mbona sikuoni?"
"geuka kulia kwako"
Sasa nilipoangalia huko kulia Daahh yaani hadi mikono ilinilegea
"ivi judi mbona unapenda kunionea hivyo... ivi nimekukosea nini haswa"
Alikua ni judith Yule alioniteka kama siku 5 hivi zilizopita... sasa ndio huyu
"jemsi? kwanza samahani kwa kukubadirishia namba.... kwani ningekupigia na namba ile ya mwanzo.. najua usingekuja"
"kwahio wewe ndio mama roda sio?"
"ndio...na nimelitumia ili usijue kama ni mimi"
"basi sasa naomba unisikilize kwa makini sana... kua leo nipo bize sana na sihitaji kutekwa tena, na kusababishiana presha ambazo hazikuepo kabisa"
Heee Mara judith alipiga magoti tena karibia anataka kusujudu miguuni kwangu
"we judi ndio nini hivyo? au ndio utekaji wa leo ulivyo nini?"
"jemsi pliizi naomba unisamee kwa yale nilioyafanya.... kwani nilikua nakutania tu siku ileee"
Judi alikua akilia kabisa tena mbele za watu na bila kujali kua wana utajiri wa kiasi gani.... Mimi hua ni mtu nisiopenda ujazo wa watu kutushangaa...
"we judi kwani vp?"
"naomba twende hotelini tukaongee vizuri pliizi"
"weeeeeee ili ukaniteke huko huko ee?"
"jemsi tafadhali sana nipo chini ya miguu yako pliizi"
Judi nilikua namchukia toka siku ile alioniteka Ila leo nilianza kumuonea huruma na kumkubalia kwenda huko hotelini...
Niliipaki toyo yangu karibu na msikiti kisha nikapanda gari la judi na kuelekea hoteli moja hivi inayoitwa THE NEW ARUSHA HOTEL ilipo maeneo ya Clock tower ( mnara wa saa )
Tulifika hotelini hapo na kuagiza msosi wa maana huku tukipiga mastori ya kawaida.... Ila judi aliniomba msamaha sana kwa lile aliolifanya kwa kuniteka na kujifanya katumwa na bosi... kumbe hakuna nini wala nini.... ilikua ni swaga zake tu... na alisema kua pale nilipozimia na kupelekwa hospitali Alishtuka sana na kuapa kua hatokaa kurudia mchezo huo tena..... Tulikaaa muda mrefu sana hapo hotelini.. Sasa tukiwa tunashushia chakula na vinywaji mara alipita mtoto mzuri kweli.. japo hajamshinda judi kwa uzuri... ila maumbo ndio wametofautiana... sasa mtoto wa kiume saa ngapi sijageuza macho na kumuangalia yule dada.....
"hee we jemsi vp?"
"Eeh? unasema? Aaahhh sory nilikua naangali ile rangi ya ukuta imependeza kweli yani"
Alishika pua huku akiniigiza kama vile nilivyoongea... tena huku akibembua mdomo
"Eti nilikua naangalia ile rangi ya ukuta... nyooo huna hata haya"
"mmhhh basi mama yaishe Eeeh.. maana nyie mkianza kusuta nyie Heeee"
"unaangaliiiiaa kwani mimi sio mwanamke?"
"sawa ni mwanamke ila si hatuna uhusiano"
"ok tuyaache hayo..... afu jemsi nimekumbuka kitu"
"kitu gani tena?"
"nikuulize?"
"uliza tu mama wala usijali Ehehe wewe tena?"
"ivi una mpenzi wewe?"
"mmhhh kwanini uulize hivyo?"
"nimekuuliza tu"
"mmhh ndio ninae"
"Eti nini?? basi tutaonana kesho"
"aaaahh sasa unaenda wapi judi?"
Judi Alikua anaondoka baada ya kusikia kua nina mpenzi..
"jamani judi hata kinywaji tu hujamaliza mama"
"kamuite huyo mpenzi wako uje uendelee nae"
"hapana judi we njoo tuongee"
Sasa katika ile hali ya kumzuia asiondoke nilijikuta nimemshika kiuno Afu nimebaki nimeduaaa...... Na yeye kasimama kisha kafunga macho kabisaaaaaa
Nikajua kwa hili kosa nililofanya hapa yaani nitakula bonge la mkibao huooo..... sasa nikajiandaa kukwepa kibao kama atarusha..... Mara akafungua macho taaratibu Lakini yalikua yamelegea hayo.... Basi mtoto wa kiume nikawa nimefunika mashavu yangu ili nisinaswe kibao....
"we jemsi ivi ni kweli una mpenzi?"
Eeeee Nilishangaa kweli kwa kutonaswa kibao.... Tena sauti yenyewe ni ileeeeee ya kutafuta..... sasa nikawa natoa tu macho kama mjusi sio mjusi....
"nakuuliza jamani jemsi si unijibu basi weweee"
Jamani nimuambieje?????
0 comments:
Post a Comment