DC LUDEWA AWATAKA WANANCHI KUJIUNGA NA CHF

Mkuu wa wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Bw.Juma Solomon Madaha amewataka wananchi wilayani hapa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF)ili kuweza kutibiwa kwa bei nafuu kwa mwaka mzima kwani magonjwa hayapigi hodi yanapoingia. Bw.Madaha aliyasema hayo jana katika vijiji vya Kiwe kata ya Mawengi na Mbwila kata ya Luana wakati wa kampeni ya uhamasishaji kwa wananchi unaofanywa na viongozi wa CHF kanda ya nyanda za juu kusini kwa kushirikiana na wilaya ya Ludewa juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ambao ni msaada mkubwa katika jamii. Alisema mfuko huo unaolipiwa kiasi cha shilingi elfu kumi kwa familia ya baba na mama yenye watoto wanne wasiozidi umri wa miaka 18 kwa muda wa mwaka mmoja wa kiserikali umekuwa mkombozi mkubwa kwa jamii kwa kutumia gharama ndogo za matibabu pale mwanafamilia anapougua. Bw.Madaha alisema licha ya kuwa Tanzania kuna tatizo kubwa na ukosefu wa Dawa lakini kwa kupitia CHF Serikali inawajibika kuchangia pale ambao wananchi wameshachangia ili kupata dawa ambazo zitaweza kuwanufaisha wachangiaji tofauti na wale wanaopata huduma ya papo kwa papo. “Nasisitisha jambo hili kwa kuwa naelewa umuhimu wake kwani kwa familia yenye watu sita inatibiwa kwa kiasi cha shilingi elfu kumi kwa mwaka mzima hapo ukipiga hesabu inakuwa kila mmoja ni kama shilingi 1500 tu hivi kuna huduma ya Afya ya papo kwa papo unaweza kuipata kwa gharama hiyo nchini?”,aliuliza Bw.Madaha. Alisema kama kila familia itachangia mfuko huo basi tatizo la ukosefu wa dawa nchini litakwisha kabisa hasa zahanati za vijijini kwani mpango wa Serikali ni kuwachangia mara mbili wale ambao tayari wameonesha kuchangia katika huduma za mfuko wa afya ya jamii. Mratibu wa mfuko huo wilayani Ludewa Bw.Petrol Mahanza alisema mwamko wa jamii katika kuchangia mfuko huo bado hauridhishi kutokana na elimu ndogo waliyonayo kuhusu jambo hilo hivyo kupitia kampeni hiyo ambayo itafanyika kwa muda wa siku 10 inaweza kusaidia kuwahimiza wanajamii kujiunga nao. Bw.Mahanza alisema bado familia ambazo zilichangia mwaka uliopita na hazikuugua zinahoji matumizi ya fedha zao jambo ambalo sio sahii kwani michango hiyo ni ya mwaka mmoja mmoja na kila mwaka familia inatakiwa kuchangia upya. Aidha meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini Bw.Emmanuel Mwikwabe alisema Serikali inampango mzuri wa huduma za Afya kwa wananchi wake hivyo kila familia inapaswa kuchangia ili kunufaika na mpango huo ambao hutolewa nyongeza ya fedha ili kuwaunga mkono kwa wale waliochangia. Bw.Mwikwake alisema katika mpango huo wa mfuko wa afya ya jamii licha ya mchangiaji kupatiwa dawa pia pesa aliyochangia inatumika pale anapohitaji vipimo na hata rufaa kutoka katika zahanati mpaka hospitari ya wilaya bado familia itatumia kiasi hicho cha shilingi elfu kumi. Alisema mpango huo ulianzishwa hapa nchini mwaka 2001
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: