AKWAYA WAPANIA KUPUNGUZA TATIZO LA UTAPIAMLO LUDEWA
Shirika lisilo la kiserikali la AKWAYA linalojihusisha na shughuri za kijamii kwa Wagane,Wajane na Watoto yatima wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe limeanza kutekeleza mpango wa kupunguza tatizo la utapiamlo ambalo limekithiri wilayani hapa kwa kutoa elimu kwa wazazi kuweza kufanya matumizi bora ya chakula.
Akiongea na wananchi katika tamasha lililoandaliwa na shirika hilo jana Ludewa kijijini Mkurugenzi wa AKWAYA Bw.Samwel Mputa alisema wialaya ya Ludewa imejaliwa kuwa na rutuba nzuri inayostawisha mazao ya chakula aina zote lakini inashangaza kuona hali ya utapiamlo iko juu.
Bw.Mputa alisema mpaka sasa takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya 52% ya watoto waishio mkoani Njombe wanatatizo la utapiamlo,hali hiyo inasababishwa na wazazi kushindwa kupanga matumizi bora ya chakula kwani muda mwingi wamekuwa wakiwaacha watoto wajihudumie wakati wao hushinda katika vilabu vya pombe.
Alisema tamasha hilo ambalo limefadhiliwa na PANATA na SAVE THE CHILDREN linalengo la kufanya uhamasishaji juu ya matumizi bora ya chakula ili kuondoa tatizo la utapiamlo kwani wako baadhi ya wazazi bado wajawa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi bora ya chakula hasa rishe bora lakini kupitia matamasha ambayo yanajumuisha vikundi vya sanaa na vyombo vya habari wananchi wanaweza kupata uelewa kuhusu rishe bora.
“Utapiamlo uko katika aina nne ambazo ni uzito pungufu chini ya kg2.5,udumavu,ukondefu na uzito chini ya ule maalumu wa kuzaliwa hali ambayo ni hatari kwa afya ya mtoto kwani hata baadhi ya wazazi hawazingatii mlo kamili hivyo kupelekea kuzaa watoto wa aina hiyo lakini sisi kama akwaya tumejipanga kupunguza na kama si kutokomeza tatizo hilo wilayani Ludewa”,alisema Mputa.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo ambaye ni mkuu wa wilaya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha katika hotuba yake alisisitiza kuwa wilaya yake haina tatizo la chakula lakini wananchi wake bado hawana mpangilio mzuri wa matumizi ya chakula bora hivyo ni vema viongozi wa vijiji na wale wahudumu wa afya ya msingi kutoa elimu hiyo wakati wa vikao vya vijiji ili kupunguza tatizo la utapiamlo.
Bw.Madaha alilimwagia sifa shirika la akwaya kwa kuanzisha mpango huo ambao utaleta mabadiriko katika jamii na kuwataka wananchi wa wilaya ya Ludewa hususani mkoa wa Njombe kuacha kujizolea sifa mbaya nchini kwani janga la ukimwi mkoa wa Njombe unaongoza pia utapiamlo siafa ambazo si nzuri kwa mikoa mingine.
Aidha meneja wa PANITA nyanda za juu kusini Bw.Aloyce Millinga aliitaka Serikali kutoa ushirikiano kwa mashirika yasiyo ya kiserikali katika miradi mbalimbali iliyaweze kushiriki ipasavyo katika kuihudumia jamii.
Alisema baadhi ya viongozi wa Serikali wamekuwa kikwazo kwa mashirika hayo pale yanapotaka kuwahudumia wananchi kwa kutokuwa na takwimu sahihi zinazohusu maendeleo ya jamii na hali ya chakula kwa ujumla.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment