DC LUDEWA AWATAKA VIJANA KUTOKIMBIA MAFUNZO YA MGAMBO
Mkuu wa wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Bw.Juma Solomon Madaha amewataka vijana wilayani hapa kutoyakimbia mafunzo ya jeshi la Mgambo kwani ni mazoezi ya ukakamavu ambayo mwisho wa siku yanakuwa ajira ya kudumu katika makampuni mbailimbali ya ulinzi.
Bw.Madaha aliyasema hayo jana katika kata ya Mkongobaki wakati wa akiyafunga rasmi mafunzo ya jeshi la Mgambo 29 akiwemo mwanamke mmoja ambapo changamoto kubwa aliyoelezwa na wakufunzi ni baadhi ya vijana kutimua mbio wakati wa mafunzo na kuhama kabisa kwa kuogopa mazoezi.
Akihutubia umati wa wananchi ambao ulifulika katika viwanja vya Mkongobaki Bw.Madaha alisema jeshi la mgambo ni muhimu sana katika ulizi wa jamii lakini inashangaza kuona baadhi ya vijana kuyakimbia mafunzo hayo ambayo ni moja ya ajira hasa kwa kipindi hiki cha uanzishwaji wa migodi ya madini wilayani Ludewa.
Alisema makampuni ya wachimbaji wa madini hayo watahitaji walinzi hivyo ni vyema vijana wakaandaliwa ili kunufaika na fulsa za ajira katika migodi hiyo na kuacha tabia ya kuwa watazamaji wa migodi yao pale walinzi wanapotafutwa wilaya nyingine na kuajiriwa kwa mishahara minono.
“Jeshi la Mgambo ni chombo cha ulinzi kinachotambulika nchini hivyo vijana mnaohitimu mafunzo haya leo mnapaswa kukaa pamoja na kufungua kampuni yenu ya ulinzi na kuisajiri na sisi tutakuwa watetezi wenu pale ambapo wawekezaji watahitaji walinzi hatutaruhusu kampunui za ulinzi za nje ya wilaya hii zikapata kazi wakati nyie mpo”,alisema Mh.Madaha.
Naye Diwani wa kata ya Mkongobaki Mh.Alfred Mtweve aliushukuru uongozi wa wilaya ya Ludewa kupeleka mafunzo hayo katika kata yake kwani vijana wa kata hiyo watanufaika na fulsa za ajira katika migodi hiyo mikubwa inayotarajia kuanzishwa na wawekezaji wa ndani ya nchi wa wale wa nje.
Mh.Mtweve alitoa sifa nyingi kwa binti pekee aliyejulikana kwa jina la Asha Mohammed kwa kuhudhuria mafunzo hayo mpaka mwisho licha ya kuwa kuna wengine walikimbia baada ya kuona ugumu wa mazoezi hivyo aliuomba uongozi wa wilaya kumfikilia binti huyo pale zinapotokea ajira za ulinzi katika ofisi mbalimbali za wilaya.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment