SITTI MTEMVU: KULIVUA TAJI LA MISS TANZANIA 2014
Siku moja baadayaMiss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu ‘kueleza’ kwenye ukurasa wake wa mtandao
wa kijamii Facebook kulivua taji hilo, waandaaji wa mashindano hayo,LinoAgency International
wamesema hawajapokea barua rasmi kutoka kwa mrembo huyo ya kulivua taji hilo.
Juzi zilizagaa taarifa kuwa mrembo huyo amelivua taji baada ya kuwapo ujumbe katika mtandao wa
facebook ambao unaonyesha umeandikwa na mrembo huyo. Ujumbe huo ulisomeka:
“Habari za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kusemwa maneno mengi yasiyo na tija juu ya
hili taji la Umiss Tanzania mpaka kusababisha nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu, kwa
roho safi nimeamua mwenyewe kulivua taji hilo na kuacha wanayeona anastahili apewe ili niendelee
na maisha yangu kwa amani, isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi.”
Hata hivyo, taarifa ambazo tumezipata zinasema, Sitti alifikia uamuzi wa kulivua taji baada ya
kushauriwa kufanya hivyo na wizara inayosimamia habari, vijana, utamaduni na michezo ambayo
ilifanya kikao juzi na Mkurugenzi wa mashindano hayo, Hashimu Lundenga na Katibu Mkuu wa
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),GodfreyLebejo
.
Inaelezwa kuwa kikao hicho kilifanyika kwa ajili ya kutafuta ukweli kuhusu suala la umri wa Sitti,
kwani nyaraka mbalimbali za mrembo huyo zinaonyesha amezaliwa Mei, 1989 hivyo ana umri wa
miaka 25 wakati moja ya vigezo ambavyo mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania anatakiwa
kuwa navyo ni kuwa na umri usiozidi miaka 24.
Wiki iliyopita Sitti aliingia kwenye kashfa zaidi ya kudanganya umri baada ya kuibuka na cheti kipya
cha kuzaliwa ambacho kinaonyesha alizaliwa Mei 31, 1991 wakati zipo nyaraka zinaonyesha
alizaliwa mwaka 1989. Nyaraka hizo ni hati yake ya kusafiria na leseni ya udereva ambayo ilitolewa
nchini Marekani.
Chanzo chetu cha habari kinasema, katika kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana
Utamaduni na Michezo yalifanyika majadiliano ya kina ikiwa ni pamoja na kulinda heshima yababa
yake Sitti ambaye ni Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu kwa hiyo mrembo huyo alishauriwa
atangaze mwenyewe kuvua taji hilo.
“Kikao cha Kamati ya Miss Tanzania nafamiliaya Mtemvu kitakaa jioni, Sitti mwenyewe ndiiye
atatakiwa kutangaza kujivua taji hilo, nadhani baadaye utatolewa msimamo wa familia ila mpango
uliopo ni Sitti aachie taji hilo,” .
0 comments:
Post a Comment