OKWI AULA SIMBA, APEWA MIAKA MIWILI

Licha ya kuwa na mwendo wa kusuasua katika mbio za kusaka ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam imeamua kumuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo mshambuliaji raia wa Uganda Emanuel Okwi. Okwi ambaye alijiunga na Simba dakika za mwisho kabla dirisha la usajili VPL kufungwa akitokea Yanga akiwa huru baada ya Yanga kukiuka baadhi ya vifungu ndani ya mkataba sasa atakuwa msimbazi hadi 2016. Akizungumza na mwandishi wetu meneja wa mchezaji huyo Abdulfatah Saleh amesema kuwa mkataba huo mpya kati ya Simba na Okwi umekuja baada ya kumalizika kwa kesi iliyofunguliwa na Yanga dhidi ya mchezaji huyo chini ya kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). “Okwi ameongeza mkataba mwingine wa kuichezea Simba, amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kesi yake na Yanga kumalizika kwa TFF kumruhusu kuichezea Simba kufuatia timu ya zamani kushindwa kutimiza makubaliano yaliyokuwepo kwenye mkataba wake. Amesema Abdulfatah. Awali Okwi alisaini mkataba wa miezi 6 akitokea Yanga kwa lengo la kusikilizia kesi hiyo lakini baada ya kushinda na kuhidhinishwa kuwa huru kuitumikia Simba na viongozi wa klabu hiyo kupendezwa na purukushani za nyota huyo sasa wameamua kumpa mkataba mrefu kidogo. Hadi sasa Okwi akiwa ndani ya michezo yote ya ligi kuu Tanzania bara Simba imcheza mechi tano, imetoa sare michezo mitano, imefunga mabao matano, imefungwa mabao matano na kufanikiwa kuvuna pointi tano na kujiweka katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara inayoendelea sasa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: