Ni kilio cha kweli bungeni au huruma ya kura 2015?


Wakati Uchaguzi Mkuu ujao ukipiga hodi,ni kama baadhi ya wabunge sasa wanakumbuka kujifunika shuka wakati kumekucha.
Hii inatokana na wengi wao kuanza kujiwekea mazingira ya kufuatilia kwa udi na uvumba utekelezaji wa miradi mbalimbali katika majimbo yao kama ilivyoahidiwa na serikali na baadhi yao wao wenyewe kutoa ahadi kwa wapigakura wao.
Hali hii imeanza kujitokeza katika kikao cha Bajeti kilichoanza mjini Dodoma Mei 6, mwaka huu na wizara kadhaa tayari zikiwa zimewasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2014/15.
Katika kikao hicho kinachoendelea, tumeshuhudia baadhi ya wabunge wakipiga kelele hata kutishia kuondoa Shilingi kutoka kwenye mshahara wa waziri mwenye dhamana kwa lengo la kutaka kupata ufafanuzi wa masuala fulani ama wahakikishiwe iwapo ahadi za serikali kuhusu utekelezaji wa miradi katika majimbo yao, zitatekelezwa.
Wizara zilizoonekana kukaliwa 'kooni’ kwa wabunge kuzibana hadi zitekeleze miradi mbalimbali ama iliyoanzishwa au kuahidiwa ni Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Wizara ya Kazi na Ajira.
Karibu kila mbunge aliyepata fursa ya kuchangia hotuba za wizara hizo, walipigia kelele utekelezaji wa miradi iliyoahidiwa majimboni kwao, lengo ni kuhakikisha kwamba wanajijengea mazingira mazuri ya uchaguzi mkuu ujao.
Mendrad Kigola, Mbunge wa Mufindi Kaskazini (CCM), anatoa kilio kwa serikali kujenga barabara za kiwango cha lami katika jimbo lake.
Hoja anayoijenga mbunge huyo ni kwamba, wilaya ya Mufindi ni kitovu cha uchumi wa taifa kutokana na kuwapo viwanda vingi vikiwamo vya chai pamoja na cha karatasi cha Mgololo.
Licha ya kuishukuru serikali kutenga bajeti ya Sh. bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za wilayani humo, Kigola anataka bajeti hiyo iongezwe ili zijengwe kwa kiwango cha lami ili kutowakatisha tamaa wawekezaji kutokana na ubovu wa barabara.
Mbunge huyo anasema barabara za wilaya ya Mufindi hazipaswi kujengwa kwa kutumia vifusi kwa kuwa hupata mvua nyingi kila mwaka na hivyo ni rahisi barabara za aina hiyo kuharibika mapema hivyo suluhisho pekee ni kujengwa barabara za viwango vya lami.
Mbunge Kigola anazitaja baadhi ya barabara anazotaka zipewe vipaumbele kujengwa kwa kiwango cha lami ni pamoja na ile ya Mafinga – Mtiri - Sawala - Mgololo na Nyololo - Igowole - Mgololo.Kwa upande wake, Mbunge wa Kisarawe, Suleiman Jaffo (CCM), amelilia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya kutoka Kisarawe - Maneromango na Mlandizi - Mzenga - Maneromango pamoja na ile ya kutoka Kibaha Maili Moja - Kisarawe.Vile vile, anashauri kujengwa kwa barabara kati ya Vikumburu na Rufiji ambayo kwa mujibu wake, itakuwa kiunganishi mwafaka na wakazi wa Kisarawe.
Hali kadhalika, Jaffo anaitaka serikali kujenga bandari kavu katika Wilaya ya Kisarawe.Kwa mujibu wa mbunge huyo, ujenzi wa bandari kavu hiyo utasaidia kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
"Magufuli ni mchapa kazi...ni jembe na jembe kweli kweli, nataraji atayafanyia kazi haya niliyoyaeleza," anamsifia waziri mwenye dhamana na Wizara ya Ujenzi, Dkt. John Magufuli na kuungwa mkono na Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makinda.
"Anafanya kazi mpaka anaconda," Spika Makinda anamsifu Magufuli.
Kwa upande wake, mbunge wa Pangani, Salehe Pamba (CCM), analilia kivuko cha uhakika kiongezwe katika jimbo lake.
Mbunge anasema takribani nusu ya wakazi wa jimbo lake, hushindwa kufika makao makuu ya wilaya kutokana na kukosekana kwa kivuko cha uhakika.
Deo Filikunjombe (Ludewa), anasema wakazi wa jimbo lake hadi walipokuwa wakisherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru, wilaya nzima haikuwa na barabara ya kiwango cha lami.
"Lakini sasa jitihada zimeanza kwani wilaya hiyo ina barabara ya kilomita moja ya kiwango cha lami.
Pia anasema upo mpango wa kujenga kilomita nyingine 50 za kiwango cha lami kati ya Njombe -Manda -Ludewa.
"Magufuli hayumo katika orodha ya mawaziri mizigo. Ni mchapakazi na kama Tanzania ingewapata mawaziri watano tu wachapa kazi kama yeye (Magufuli), basi taifa lingebadilika haraka sana kimaendeleo," anamsifu Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli.
Anaongeza, “Magufuli ni waziri wa wote kwani amezigawa barabara bila upendeleo. Karibu Ludewa Mheshimwa Magufuli na kama ukija kwetu Ludewa, wananchi wa huko watakubadilisha jina na kukuita 'Kayombo ama Mtweve."
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Susan Kiwanga, anasema licha ya Mkoa wa Morogoro kuteuliwa kuwa ghala la Taifa, lakini barabara zake nyingi hususan katika wilaya ya Kilombero hazipitiki.
Anaiomba serikali kuuangalia mkoa wa Morogoro kwa jicho la karibu kwa kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami ili zipitike msimu mzima.Kiwanga anaishauri serikali kujenga barabara za kiwango cha lami ya kutoka Ifakara hadi Mlimba na Mlimba hadi Mdeke.Vile vile, mbunge huyo anaitaka serikali kuimarisha kivuko cha Kilombero.
Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), anasema vipaumbele vya miradi ya utengenezaji wa barabara

Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment