MAAJABU HAYA: SOKWE WAGUNDUA KIFAA CHA KUNYWEA MAJI

Sokwehttp://ichef.bbci.co.uk/news/ws/590/amz/worldservice/live/assets/images/2014/07/04/140704131813_chimps_communication_512x288_chobaiter_nocredit.jpg
Watafiti wamegundua kifaa kipya kinachotumiwa na idadi kubwa ya masokwe .
Wanasema kuwa kifaa hicho ni ishara tosha kwamba masokwe wa mwituni wameanzisha tabia mpya.
Wakati kundi la Watafiti hao lilipokuwa likichukua filamu ya sokwe hao katika kituo kimoja nchini Uganda,walibaini kwamba baadhi yao wamekuwa wakitengeneza sponji la majani ambalo hulitumia kunywa maji.

Tabia hiyo mpya tayari imeanza kuenea kwa sokwe wengine.Mtafiti bingwa Catherine Hobaiter kutoka chuo kikuu cha St.Andrews anasema kuwa sokwe hao huliingiza sponji hilo katika vidimbwi vya maji na baadaye kulifyonza.
Ameiambia BBC kwamba waliona vifaa viwili vipya vinavyotumiwa na sokwe hao.
Anasema kuwa alimuona sokwe mwengine akitumia mmea wa Moss badala ya majani kutengeza sponji lake.
Mwengine alichukua sponji lililotumiwa na mwenzake na kuanza kulitumia.
Amesema kuwa ingawaje habari hizo zinaonekana kama zisizokuwa na maana,masokwe hawajakuwa na tabia kama hiyo.
CREDIT: BBC/SWAHILI


Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: