DEREVA TOYO sehemu ya 5 a

DEREVA TOYO sehemu ya 5 a inaendelea "samaani dada naomba unieskoti hadi pale lami tu... maana huu mtaa wenu siujui vizuri" Nilidanganya tu ili nipande tena kwenye gari, Maana hapo ndio ilikua mwisho wangu "ok twende" Wee nilifurahi kimoyo moyo mimi duu Sasa tukiwa njiani swaga ni zile zile za kuangaliana kwenye kioo Sasa nikawa nataka niseme kitu lakini nahisi atakataaaa..... lakini potelea mbali mimi nasema tu "dada eeh?" "sema?" "eti umejifunza gari lini?" "siku nyingi tu toka nikiwa mdogo" Aiseeee mimi ni fala duuu Yaani hata sikutaka kumuuliza hivyo ila vimekuja tu mdomoni.... Yaani mimi ni fala tena zaidi ya fala kwa jinsi nilivyo domo zege...... ENDELEAA Nilijiona ni mjinga sana kwa kuropoka mambo ya gari na wakati hayaniusu. Lakini mtoto wa kiume hua nimejaaliwa sana kwenye upande wa macho na mikono.... kwani hua nikikaa na demu karibu afu kama anaonekana ni wakushawishi tu... hua natumiaga macho na mikono UNAJUA KUFANYA HIVYO ITATEGEMEA NA MWANAMKE ALIVYO SIRIASI... MAANA KUNA MIDEMU MINGINE IPO SIRIASI MPAKA KIDUME KINAOGOPA KUTOKEA..... AFU NYIE WANAWAKE HEBU PUNGUZENI USIRIASI BWANA KWANI HUA MUNATUOGOPESHA KUWATOKEA....... SASA HUYU JUDI YEYE ALIKUA HAYUPO SIRIASI..... YAANI SIO MKIMYA WA KUSEMA LABDA UTAMUOGOPA....... ILA SEMA TU NI UDOMO ZEGE WANGU NDIO UNANISUMBUA MNO...... MAANA SIJUI HATA KUTONGOZA YANI DUUUUU HAPA KAZI IPO Niliona potelea mbali kama ni mbaya wacha iwe mbaya tu Nilijipanga vizuri ili niongee mara nikaskia "si ndio hapa tumefika?" Nikaona nikisema bado nitaonekana boya, maaana hapa ndipo nilipomwambia anifikishe "Eehh ndio hapa" "poa basi tutaonana" "Eeeee ok sawa sawa" Nilikua kama nina wenge hivi, Maana mtoto ni mzuri afu kwa mashavu ( matajiri ), Niliona huu ni ufala kabisa yaani kitoto kizuri hivi sijakiomba hata namba ya simu??? Aaaaa Haiwezekani bwana bora niondoke hata na namba za simu aiseee "Samaani judi kwani hata namba za simu hatupeani jamani?" "tehetehe bwana simu yangu mbovu" "aaahhh sasa unaniongopea judi" "kweli vile ila kesho nitanunua nyingine" "Aaaaaa basi nipe namba then nitakucheki kuanzia kesho" "sasa utachukuaje namba na wakati sina simu?" "ok poa ila zakwangu zipo pale pembeni ya picha" "ok nitakutafuta kama nikiwa nataka picha" "aaaaa judiiii sio picha tuu hata tusalimiane na kupeana mahai tu" "ok poa" Basi nilishuka kwenye gari na kuondoka zangu maana alinieskoti kidogo Daahh yaani toka nianze kazi ya picha sijawahi kushika elfu 50 kwa mkupuo, Nilifika hadi nyumbani huku nikiwa nimebeba kidumu cha mafuta ya kula ili nikampooze mama kwa kile alichokiona baina yangu na rey, Nilifika hadi nyumbani na kuingia mpaka ndani huku kidumu kipo mbele mbele ili kionekane na mama, "shkamoo mama?" Hee ulitoka msunyo mrefu huooo "mschiuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu" Lakini bado nikawa najibalaguza balaguza pale "mama nimekuletea mafuta" "kwani nilikuambia nataka?" "lakini kwani kosa langu ni lipi mamaa?" "wewe juzi nilikuambia nini?" "ulisema nisiwe na wanawake wa kisasa" "sio wakisasa tu hata wa zamani sitaki" "sawa nimekuelewa ila mwenyewe si umeona nimemkataaa mama" "yaani siku nikikuona una mwanamke wewe" "lakini kwanini mamaa?" "wanawake wa siku hizi ni waongo sana nahofia magonjwa mwanangu" "basi mama nimekuskia" "haya ulikua unasemaje?" "nimekuletea mafuta ya kupikia" "asante na ubarikiwe" "hahahahahaha kumbe ulikua unayatamani" "hehehehe yaani hapa nilikua naomba usije ukayarudisha maana wewe hazikutoshi kabisa" "na ningerudi nayo" "na usingekula humu ndani" "eeee kisa?" "si umerudi na mafuta dukani" "duuuu kweli nyie ni noma kweli" Mara baba kaingia "shamoo mzee?" "marahaba vp?" "safi tu" Nilimpokea alichobeba kisha nikaingiza ndani, na kutoka nje Maana wazee wanaongea yao na hayaniusu "we jemsi unakwenda wapi tena?" "nipo kwa hapa nje mzee" "hebu nikutume kwa baba rehema umwambie nipo nyumbani" "sawa mzee" "chapu chapu sasaa" Daahh mzee kanipa mtiani wa kwenda kwakina rey... duuuuu kazi ipo leo Kwakina rey na kwetu sii mbali ni hatua kadhaa tu umefika.... Nilifika kwakina rey lakini nasita kugonga geti... "ngongongongo" Niligonga mgeti wao huo "naniii?" Ilikua ni sauti ya rey ndio iliniuliza "ni mimi jemsi" "unataka nini?" "tafadhali sana nimeagiziwa na baba huko kwa baba ako" "ili iweje?" "aaaahhh sasa maswali gani hayo rey?" "yaani jemsi nakuchukia wewe" "lakini rey bifu letu ni letu...na ya wazazi ni ya wazazi tu.. kwahio naomba ufungue ili nifikishe ujumbe" Mara akafungua Geti kisha nikaingia mpaka ndani na kumuona baba yake rey... "shkamoo mzee?" "marahaba ujambo?" "sijambo tu.... Aaahh mzee nimeagiziwa na mzee wangu" "anasemaje?" "Ameniambia tu nikuambie kua yupo nyumbani" "aaaaahhh OooKeeeee nimekumbuka, Sasa mwambie nakuja sawa?" "sawa mzee" Basi mtoto wa kiume sikukawia kutoka nje..... Maana rey alikua yupo getini afu kavimba huyo duuu "asante na kwaheli eeh?" Nilijaribu kumuaga mtoto rey lakini akaendekeza bifu tu, "sitaki afu usinizoee jemsi Oohoo we haya tu" Nikakosa lakuongea maana ni kweli nilimkosea ila ni kwasababu ya mama angu... Inatendelea 5b
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: