DEREVA TOYO sehemu ya 4 b
Inaendeleleaaa,,,
"heeee una mke wewe?"
Aliuliza yule judi
"ndio tena mkubwa huyo yaani tena nikichelewa hapa ni kesi"
Basi walikua wanacheka kweli yani. maana nilianza kuwapa utani wa hapa na pale
"sawa naondoka basi"
Nilikua naongea huku nikijinyoosha nyoosha vidole.. mana hii nyumba imejaaliwa kwa watoto,
"ok sasa nikurushie kwenye M-pesa?"
Aliniuliza huyu mtoto judith huku akichokonoa simu yake... bonge la simuuuu daa utafikiri bibiria vile
"Apana kwani laini yangu imefungiwa M-pesa"
Nilimdanganya ili nitoke nae mpaka kwa wakala nje......
"kwanini imefungiwa?"
"mmhh sijui"
"au usikute we ni mkorofi wewe"
Aliongea huku akicheka akimaanisha ni utani kwa anachokiongea
"ok wacha nikutoe na gari ili nikakutolee pale diukani sawa?"
"sawa"
Sasa hivyo ndivyo nilivyokua nataka ili nijaribu bahati yangu...
Basi tulipanda gari na yeye mwenyewe ndio dereva. Mlinzi alifungua geti kisha tukatoka mpaka nje
Sasa kinguo alichovaa ni kama TENTEMENTE ila sio kwani hio ilikua ni fupi sana afu ukicheki mtoto ni cheupe pyeee
"hee hii nguo ndio unatokayo hadi nje?"
Nilimuuliza huku nikiwa kama namuangalia mapajani
"ndio.... kwani vp?"
"nmmh naona ni fupi sana"
Mara tukagongana macho kwa kutumia kile kioo cha pale juu ya dereva.. maana mimi nikiangalia kioo kile basi nitamuona macho... na yeye pia hivyo hovyo......
Sasa kila mtu anamuonea aibu mwenzie kwa maana wote ni lika moja
Sasa tatizo mimi ni domo zegejamani Maana mtoto keshakaa mkao wa kutongozwa kabisa maana namuona anacheka cheka tuuuu.....
Nilijitahidi kumuuliza kitu japo nakijua
"ivi unaitwa nani vile?"
Niliuliza huku naangalia mbele ili nisione aibu sana
"we nawe inamana hujaskia pale shangazi alivyonitaja?"
"mmhh Aah nimesahauu"
"mmhhh haya naitwa judith"
"waaaoo jina zuri"
"mhm asante"
Sasa mtoto wa kiume kimya kikatanda sina hata neno la kuongea..... Daaahhh ama kweli udomo zege kazi duuuu
Mara tukafika dukani kwa wakala wa voda ili atoe pesa anipe.
"ni shing ngapi vile?"
"ni elfu 20 tu"
"mbona ni ndogo hivyo?"
"ndio kwani alishanipa elfu ishirini"
"ok poa"
Alitoa pesa pale kisha akanipa shilingi elfu 50 kamili
"hii yote ni ya nini?"
Nilimuuliza huku nikiziangali pesa zile
"nimekupa tu, maana mimi nilijua unadai kitu kama laki hivi, kumbe ni elfu 20 tu? na hizo nimekuongezea kwa kazi nzuri"
Aliongea huku akipanda gari na kuliwasha kwa kuondoka.....
Nilijiona fala kweli yaani mtoto lika langu huyu nashindwa kumsaundisha??? Aaahh Hapana wacha nifanye kitu hapa
"samaani dada naomba unieskoti hadi pale lami tu... maana huu mtaa wenu siujui vizuri"
Nilidanganya tu ili nipande tena kwenye gari, Maana hapo ndio ilikua mwisho wangu
"ok twende"
Wee nilifurahi kimoyo moyo mimi duu
Sasa tukiwa njiani swaga ni zile zile za kuangaliana kwenye kioo
Sasa nikawa nataka niseme kitu lakini nahisi atakataaaa..... lakini potelea mbali mimi nasema tu
"dada eeh?"
"sema?"
"eti umejifunza gari lini?"
"siku nyingi tu toka nikiwa mdogo"
Aiseeee mimi ni fala duuu Yaani hata sikutaka kumuuliza hivyo ila vimekuja tu mdomoni....
Yaani mimi ni fala tena zaidi ya fala kwa jinsi nilivyo domo zege......
0 comments:
Post a Comment