DEREVA TOYO sehemu ya 4 a

ILIPOISHIA JANA Sasa mtoto wa kike alikua kavaa jishuka tu peke yake... sasa si nikaona upaja wa mtoto....Na nanii ikaanza kusimama. Sasa rey kaniona kua nalikazia macho paja lake lakini harudishii nguo tena ndio anazidi tu kulifunua.. Nikamkonyeza na kumuambia afunike.... sasa kumbe hakunielewa yeye alijua namuita Saa ngapi hajaja mpaka karibu yangu na kuanza kudodosa macho mdondoko...nami nikaanza kulainika taratiiibu Mara nikaskia naitwa na mama angu "we jemsi pumbavu wewe, Yaani we mtoto husikii wewe" "we rey sogea mama angu huyoo" "mi nataka ajue uhusiano wetu" "Eti nini?" Mungu wangu rey ataniletea majanga sasa.... Afu mtoto ndio kanishika kiuno vibaya mno.. na mama angu anatoa macho huyo duu ENDELEAA Sasa nilimchana laivu rey ili tu asinigombanishe na mama angu. "nishasema sikutaki na uniache" Niliongea kwanguvu mpaka majirani walitoka na kuanza kurundikana, Mpaka rey aliona aibu kwa kukataliwa na uzuri wake wote, Pia watu wengi walishangaa ni kwanini nimemkataa rey? Na ukimuangalia rey ni msichana pekee anaevutia mtaani kwetu, yaani hana mshindani kabisaa.... Baada ya kujaza watu pale niliamua kuondoka na kumuacha na watu wake, Ila moyoni sikupenda kumuambia vile Kwahio ni mama ndio kanishinikiza japo hakuniambia nimuambie vile, Nilitoka pale huku nikifikiria kuusu lile tukio lilitokea tokeaje pale. Maana hata mi mwenyewe sikulitegemea kabisa kama ningelimuambia vile...... Sasa nikajikuta nimeharibu kabla sijapata nilichokitaka, Maana nilitaka kujua wanapoishi wale watu niliowapiga picha, Kwasababu siwajui kwa maana si nilikutana nao tu ukumbini, Ilibidi ninyooshe goti tu hadi kule gaden rose, Kwani huenda nikapata hata namba zao za simu. Nilifika geden rose hapo na kupanda hadi kule ukumbini walipokua jana, Ila sikukuta mtu yeyote...... Basi nikawa nashuka kwa ngazi taratibu ili tu nikamuombe msamaha rey, maana ndio anajuana nao, Sasa nilipokua nashuka niliona sura moja ambayo ilikuepo jana na hata kwenye picha ninayo "we dada subiri kidogo" "nani mimi?" "ndio ni wewe" Basi nikashuka fasta fasta na kusalimiana nae.. "habari yako dada?" "safi tu zakwako?" "aaahh nzuri tu" "Enhe ulikua unasemaje?" "ivi hunikumbuki?" "mh apana sikukumbuki kabisa kaka angu" "aaahh mimi ni yule mpiga picha wa jana katika sherehe yenu" "aaaaAAAAAaa wewe ndio ulioletwa na rey eeh?" Dada huyu alinikumbuka vizuri sana tena bira shaka alifurahi zaidi "ndio ndio" "sasa picha ziko wapi?" "ndio nilikua nafanya mpango wa kufika kwa mwenye sherehe ili nimpe picha zake" "kwani hupajui?" "aahh dada sasa nitapajuaje na wakati hata hapa ukumbini penyewe nililetwa?" "ok hata mimi ni mwanafamilia wa huyo mama sasa sijui utaweza kuniamini unipe hizo picha?" "mmmmh labda twende wote ili niwe muaminifu zaidi" "ok twende basi" Sasa mtoto wa kiume nilipanda gari la huyo dada na kuondoka DADA HUYU NI MDADA WA MAKAMO YAANI KAMA ANGELIKUA NI DADA YANGU BASI ANGEKUA NI MARA MBILI YA DADA YANGU.... NAMAANISHA KUA HUYU DADA NI WA HESHMA KIDOGO, SEMA TU SISI VIJANA WA SIKU HIZI HATUNA HESHMA HATA KIDOGO... MAANA ALIPASWA APEWE SHKAMOO YANGU... ILA KWA UJANA WA KIJINGA.. NIKAMWAMBIA HABARI YAKO ETI KISA ANA UMBO LA KISCHANA NA PIA KAUMBIKA KWELI....... Basi kwakua tulitumia usafiri wa gari yake hivyo tulifika mapema mno "kwanini usingemuambia rey akulete?" Duuuu sijui nimjibuje maana mi dio najua nini kinaendelea bana yangu na rey "aaahhh rey yupo bize sana na kazi za mama ake" "ooohh sawa sio mbaya pia" Nikajikuta najiskia afadhali kidogo kwa moyo wangu, Sasa mdada akapiga honi kisha akafunguliwa geti kuu, Na tukaingia ndani..... Duuu kweli familia yao ni kubwa kweli, maana nilikutana na watu haoo duu Tulishuka pale huku mimi nikiona ona aibu ya hapa na pale, Maana kuna watoto hao Ayaaaaa ni shidaa "mambo mkaka?" Walianza kunisalimia wenyewe watoto wa watu "poa tu" Walinitengea kiti kisha nikakaa vizuri na wao wakajikusanya ili waone picha zao, Basi nami nikatoa mkoba wangu na kutoa picha zao zote... "haya mzigo wenu huo... naa naomba muniitie huyo mama enu animalizie pesa yangu" Niliongea hivyo kisha wakapokea na kuanza kuziangalia "jamani picha zimetoka vizuri hizo" Waliongea kila mmoja kusifia ila mi macho yangu yalikua kwa wadada wawili wazuriiii balaaa.... Walioponiangalia tu na wakaangalia chini kwa aibu ya kugongana macho. "huyo mama enu yupo wapi?" Niliuliza kwa wote ila yule mmoja mzurii ndio alinijibu "kama ni pesa nitakupa mimi usjali" Yaani mtoto akiongea huku vimacho vinapepesa hadi raha yani.. "sasa jamani nataka kuondoka" Niliwaaga huku nikiamka kiuvivu fulani hivi..... kisha nikamuuliza yule mdada niliokuja nae "dada vp hunirudisha hadi mjini?" "mmhh bwana sijiskii kurudi tena kwani naskia usingizi huoo" Yule dada alionileta ndio alisema hivyo. Nami nikajisemea tu kwa sauti "duuu na mimi hela siiinaa" "hela huna? si utapewa na judi sasa hivi" JUDI NDIO YULE ALIENIAMBIA ATANIPA PESA BADALA YA BIMKUBWA WAKE..... "mmhh sasa hio nikipewa naipeleka nyumbani kwa mke wangu" "heeee una mke wewe?" inaendeleaaaaaa,,,,,4b
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: