GARI LA JWTZ LAPINDUKA WILAYANI MAKETE MKOANI NJOMBE
Mkazi mmoja wa Wilaya ya Makete Mkoani Njombe Bi.Tumulikwe Sanga (49) amejeruhiwa baada gari ya jeshi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kugonga kalavati na kupinduka katika kijiji cha Tandala wilayani hapo
Taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fugence Ngonyani imesema kuwa tukio hilo lilihusisha gari lenye namba 5968 JWTZ aina ya Land Ashoke mali ya kikosi cha KJ(911 ambayo ilikuwa na watu 17 ambapo watano kati yao ni askari na 12 ni raia wa kawaida.
Gari hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na askari mwenye namba MT 84276 CPL Munishi Antony wa KJ 911 Dodoma lilikuwa limetoka Dododma kuelekea Makete ambapo lilifeli breki kwenye mteremko na kusababisha ajali hiyo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi lilitoa wito kwa madereva kuwa makini pindi wanapoendesha vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuvifanyia ukaguzi kabla na baada ya safari ili kuepusha ajali zisizo za lazima.
0 comments:
Post a Comment