UNUNUZI WA MAHINDI LUDEWA WAINGIA DOSARI


Ununuzi wa mahindi kwa Wakulima wadowadogo wa wilayan ludewa mkoani njombe umeingia dosari siku ya juma mosi baada ya wahusika wa kupima mahindi kutoka shirika la chakula la taifa NFRA kugoma kwa sababu walitaka kupima mahindi ya mfanya biashara mwenye jumla ya gunia mia nane.
Wakiongea kwa jazba kubwa wakulima wadogo wadogo katika ghala la kuifadhia mahindi lililopo katika mtaa wa ludewa kijijini kata ya ludewa wamesema kuwa messikitikitishwa na jinsi utaratibu wa upimaji wa mahind jinsi unavyofanywa kwan wanaopima ni viongoz wa halmashauli pamoja na wafanya biashara wakubwa ambao walinunua mahindi kutoka vijiji vya jiran kwa bei nafuu na kisha wao kuja kupima mahindi hayo mara nne kwa wakala wa taifa wa chakula NFRA .
Upimaji wa mahindi katika wilaya ya ludewa ulianza siku ya juma tano ya wiki na kufunguliwa na mkuu wa wilaya ya ludewa bw.juma solomon madaha ambapo aliahid haki kwa kila mkulima kabla siku ya pili kuwageuka wakulima na badala yake wao viongoz wa halmashauli ndio waliokuwa wa kwanza kupima mahindi.
Kufuatia hali hiyo wakulima hao wadogo walilazimia kutafuta nguvu zaid kutoka serikali ambapo walimtafuta mbunge wao wa jimbo la Ludewa ila hakupatikana kwa kuwa yupo kikaz nje ya nchi, baaada ya kuona jitiada hizo zimekwama kwa umoja wao waliweza kumtafuta naibu wazir wa chakula na akawaahid kufika wilayan hapo muda wowote kuanzia sasa.
Usikose kuendelea kufuatilia mtandao huu kujua wazir kaasema nn alipowasili ludewa.

Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment