NAIBU WAZIRI WA CHAKULA NA USHIRIKA MH.GODFREY ZAMBI ATAKA HAKI ITENDEKE UNUNUZI WA MAHINDI LUDEWA.

Naibu waziri wa chakula na ushirika Mh.Godifreyi Zambi amefanya ziara ya kushitukizaa katika ghala la kuifadhia mahindi la ludewa kijijini lilipo wilayani ludewa mkoan njombe kufuatia malalamiko ya wakulima wadogo kutengwa katika ununuzi wa mahindi kutoka kwa wakulima.
Akiongea na wananchi waliokusanyika katika eneo hilo la Ludewa kijijini naibu waziri wa chakula na ushirika mh.zambi amewataka wakala wa taifa wa chakula NFRA kuhakikisha wanatenda haki kwa wakulima wodogo ili kuondoa malalako kwa wakulima hao.
Wananchi hao walitoa malalamiko yako kufutia utaratibu wa kuuza mahindi jinsi ulivyokuwa unaendelea kwa kupima mahindi ya viongoz wa halmashauli na wafanya biashara wakubwa ambao walinunua mahindi kwa wakulima kwa kuwanyonya na wao kuuza kwa wakla wa taifa kwa bei nafuu.
Akijibu tuhuma hizo mkuu wa wilaya wa ludewa Bw.Juma solomon madaha alisema kuwa lawama hizo zinatokana na mfanya biashara mmoja kupima magunia 1500 ya mahindi .
Pia naibu wazir ameongeza kuwa ni vyema kuanza kupima mahindi ya wakulima wadogo ambao wana magunia yasiyozidi 50 baada ya hapo waje wakulima wakati na kisha wakubwa pamoja na wafanya biashara.
Naye diwan wa kata ya ludewa Mh.monica mchiro kwa nafasi yake alimwomba naibu wazir wa chakula na ushirika kuongezewa tani za ununuzi wa mahindi kufuatia uwingi wa mahindi waliyonayo wakulima.
"mh naibu waziri haya maindi unayoyaona hapa ni kidogo kuliko mahindi yaliyo nyumban mwa wananchi tunaomba msaada wako mahindi haya yaweze kununuliwa yote"alisema mh mchiro.
Kwa upande wake naibu wazir akijibu ombi hilo alitanabaisha kuwa mwanzo kituo hicho cha Ludewa kijijini walipangiwa tani 3000 kutoka na wingi huo wameongezewa tani 2000 na kuwa jumla ya tani 5000 ambazo zitanunuliwa katika kituo hicho.
Kwa upande mwingine amewatoa wasiwasi wakulima hao kuhusu soko la mahindi pamoja na kueleza kuwa soko litapatikana kwa wakala wa taifa wa chakula na kama yatabaki wataluhusu walanguzi..
Nao wananchi wa wilaya ya ludewa wamemshukulu mbunge huyo na naibu wazir kwa ushupavu wake na wamemtaka awe na moyo huo wa kuwatendea haki wananchi bila ya kuchagua wa kuangalia langi na ukabila.
Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment