jivunie ludewa na historia yake

Kata ya Manda
Nchi Tanzania
Mkoa Iringa
Wilaya Ludewa
Idadi ya wakazi
- 8,084
Mandani jina la kata ya Wilaya ya Ludewakatika Mkoa wa Iringa, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ina wakazi wapatao 8,084 waishio humo. Zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumaniilijulikana kwa jina laWiedhafen [1]ikawa kitovu cha Nyassa ya Kijerumani kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Wajerumani walichagua mahali pa Wiedhafen-Manda kwa sababu ilikuwa mwisho wa njia ya misafara kati ya Kilwana Ziwa Nyassa na kuwa na bandari asilia.
Manda iko kwenye mwambao wa Ziwa Nyasakaribu na mdomo wa mto Ruhuhu, ina vivutio vingi ikiwemo ufukwe maridhawa wa ziwa Nyasa. pia kuna Kanisa la Mt Thomaso na pia bandari ya kale ya Manda-Wiedhafen.
Wenyeji wa kata ya Manda ni wamanda na lugha yao ya asili ni kimanda. Vyakula vya asili vya wakazi wa Manda ni Ugali wa muhogo na samaki. Ngoma za asili za wakazi wa Manda ni Mganda, Kihoda na ligambusi.
Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment