KAMPUNI YA BOIMANDA YAENDELEA KUIPANUA BARABARA YA LUPINGU,LUDEWA
Mitambo ya kampuni ya Boimanda ikiendelea na upanuzi wa barabara ya Lupingu kuja Ludewa mjini
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka kituo cha redio Best fm kilichoko wilayani Ludewa wakiwa Muhandisi wa kampuni ya Boimanda Bw.Taji aliyevaa shati la mistari wakiangalia upanuzi huo wa barabara
mtambo ukiwa kazini
Barabara ya Lupingu inaendelea kufanyiwa ukarabati mkubwa kutokana na barabara hiyo kuwa na milima mikali na kona nyiki ambazo ni chanzo cha ajali nyingi zinazogharimu maisha ya watu.
Hivi karibuni katika barabara hiyo ndiko ilikotokea ajali ya basi aina toyota costa ijulikanayo kwa jina la DMX iligoma kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma ndipo dereva alipoamua kuligongesha ukutani na kupinduka ambapo lilisababisha kifo cha Diwaniccm wa viti maalumu kata ya Lupingu Mh.Prisca Kayombo (Zarutha) kutokana na milima mikali.
Muhandisi wa kampuni ya Boimanda ambayo inafanya ukarabati wa barabara hiyo Bw.Taji alisema kuwa Serikali kupitia wakala wa barabara Tanroad wameipandisha hadhi hiyo barabara na kuanzia sasa itakuwa ikijengwa na Tanroad badara ya Halmashauri.
Bw.Taji alisema mpaka sasa tayari Serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 900 ambazo zitafanya kazi ya upanuzi na uwekaji changalawe katika maeneo korofi ili iweze kupitika katika misimu yote.
"tumepewa kazi ya kuipanua barabara hii na kuweka changalawe katika maeneo korofi ili iweze kupitika katika vipindi vyote kwani awali barabara hii ilikuwa chini ya Halmashauri ya wilaya ya Ludewa lakini kwasasa imechukuliwa na Tanroad ninauhakika itakuwa nzuri zaidi na itapunguza ajali",alisema Taji.
Bw.Taji aliwataka madereva wanaoendesha magari yanayoelekea Lupingu kuwa na mwendo wa kistaarabu wenye umakini mkubwa kutokana na barabara hiyo kuwa na kona nyingi zinazoweza kusababisha ajali mbaya na kugharimu maisha ya watu.
mwisho.
Jivunie kuwa mwana ludewa
Blogger Comment
Facebook Comment