Machimbo ya madini vinu vya Mills njiani kwenda kufungwa toka bandarini

dewa kumekucha: Machimbo ya madini vinu vya Mills njiani kwenda kufungwa toka bandarini


Mitambo hii imekwama kufikisha maeno husiku huko Ludewa ikisubiria ukarabati wa barabara toka Itoni hadi Manda na kutoka Mkiu hadi Liganga ili mitambo hiyo iwezi kufishwa maeneo husika yanahitaji barabara pana kutosha.

MACHIMBO YA CHUMA LIGANGA NA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA

FURSA ZINAZOKUJA NA UWEKEZAJI WA MRADI WA CHUMA NA MAKAA YA MAWE LUDEWA


Wajasiriamali wa Wilaya ya Ludewa na watanufaika na uwekezaji mkubwa wa mradi wa migodi ya chuma na makaa ya mawe unaotarajiwa kuanza mapema mwakani. Mradi huo mkubwa wa madini ya chuma uliopo katika kijiji cha Liganga wilayani Ludewa na Makaa ya Mawe yaliyopo katika kijiji cha Mchuchuma Nkomang’ombe wilayani humo ni miongoni mwa miradi mikubwa nchini itakayoleta maendeleo ya kasi katika Taifa hili linalosherehekea miaka takribani 50 ya uhuru wake.

Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka china katka Kampuni iiliyoingia Ubia na NDC zinasema kuwa aina hiyo ya uwekezaji utakaoanza kwa kuwa na wafanya kazi elfu tano {5000} katika machimbo ya chuma na elfu tano {5000} katika machimbo ya makaa ya mawe huwa na tabia ya kwavutia zaidi ya wakazi milioni moja {1,000,000} katika mazingira na maeneo ya mradi. Kwa maana hiyo basi, mradi huo ukikamilika utawavutia wakazi zaidi ya milioni moja katika maeneo yanayozunguka mradi huo.

Madhumuni ya makala haya ni kujarifu kuwaarifu na kuwahabarisha vijana na wajasiriamali wanaoishi katika wilaya ya Ludewa na mikoa ya jirani jinsi watakavyonufaika na uwekezaji huo mkubwa kwani imekuwa ni tabia sasa kwa baadhi ya watu kuwa walalamishi zaidi kuliko kufanya tathmini ya fursa zitakazokuja na uwekezaji huo mkubwa kuliko uwekezaji wowote nchini ukitoa uwekezaji katika mradi wa TAZARA ambao pia umejengwa na kudhaminiwa na nchi ya China.

Je, ni namna gani fursa zinaweza kutazamwa katika uwekezaji huo mkubwa? Hapa chini ni mwanzo tu wa namna ya kuanza kuziangalia fursa zitakazokuja na uwekezaji wa mradi wa chuma na makaa ya mawe Nchini.
1. Kutakuwa na wafanyakazi elfu kumi ambao wataajiriwa na kama kila familia itakuwa na watu watatu watatu tu nyumbani basi tunaongelea ujio wa watu wapatao elfu thelathini {30,000} watakaokuwa na mashikamano ya moja kwa moja na migodi na ajira. Hivyo sisi tuwatizame wafanyakazi hao elfu kumi tu na baadhi ya mahitaji yao ya moja kwa moja. Kama ifuatavyo:

- Kila mfanyakazi atahitaji maziwa lita moja kila siku, mayai mawili, na nusu kuku kila siku. Bila kuangalia mahitaji mengine kwa jumla mahitaji yatakuwa kama ifuatavyo:
i. Kutakuwa na mahitaji ya maziwa lita elfu kumi {10,000} kila siku
ii. Kutahitajika mayai elfu ishirini {20,000} kila siku
iii. Kutakuwa na mahitaji ya Nyama za kuku na kuku elfu tano {5,000} watakuwa wanahitajika kila siku.

Hiyo ni sehemu ndogo tu ya fursa za uwekezaji zitakazokuja una machimbo makubwa ya chuma na makaa yam awe. iMADS imefanya tathmini Ludewa na kugundua kuwa hakuna kuku wa kienyeji wala wa kisasa wa kutosha, na bei ya kuku mmoja inaanzia shilingi elfu 13 hadi elfu 20 kutegemea muuzaji na uzito wa kuku. Hakuna taxi hata moja, hakuna hotel za kisasa, hakuna nyumba za kupangisha wala maeneo ya starehe.

Hadi iMADS inaondoka wilayani Ludewa, kulikuwa na shamrashamra za kuweka sahihi mikataba baina ya wakandarasi na TANROADS ya kukarabati na kupanua barabara ili kutengeneza kiwango cha changarawe kwa dhumuni la kuwezesha vifaa vya wawekezaji vyenye uzito wa hadi tani 150 na urefu wa hadi mita 15 ambavyo vitahitaji barabara ya aina yake kuviwezesha vipite salama hadi migodini.

Makala hii itaendelea ili kuonesha fursa zaidi zitakazokuja na uwezi wa migodi ya chuma na makaa yam awe Ludewa.

Source: UjasiriMali na iMADS
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment