WANANCHI WA LUVUYO WILAYA YA LUDEWA WASITISHA UAMUZ WAO WA KUHAMIA JIMBO LA NJOMBE.

Wananchi wa kijiji cha Luvuyo kata ya Madope Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe leo wampokea mbunge wao Mh. Deo Filikunjombe halimaarufu kama jembe jinsi ambavyo anafahamika wilayaan hapa kwa usafiri wa Ng'ombe ikiwa ni ishara tosha ya kumpongeza kwa jitiada mbali mbali za maendeleo ya wilaya ya ludewa haswa katika upande wa kuboresha barabara kila kona ya wilaya hii vijiji pamoja na Kata mbalimbali ikiwa pamoja na Luvuyo. Ikumbukwe kuwa ubovu wa barabara ndan ya wilaya ya ludewa ambayo awali ilikuwa kero kubwa Kwao na wilaya nzima kwa muda mrefu kabla ya mbunge jembe kuleta mabadiliko kila kona, pia siku za hivi karibun wananchi hao walikuwa na lengo la kutaka kuomba kuhamia jimbo la Njombe kusini kutoka na kijiji hicho cha luvuyo kusahaulika katika shughuli mbali mbali kwa wilaya ya ludewa,kutokana na jitihada za mbunge wao jembe kila mmoja amesema hahami mtu na watabaki jimbo la Ludewa baada ya neema kubwa kuonekana kutoka kwa mbunge wao deo filikunjombe. Pia wananchi hao wa luvuyo wameongeza kuwa toka nchi ipate Uhuru hakuna mbunge aliyejitolea kama Filikunjombe na hivyo hawa hitaji mbunge mwingine mwaka 2015 ili wilaya iendelee kupiga hatua za maendeleo. Mbali ya wananchi kumpongeza kwa Ujenzi wa barabara hiyo pia wanafunzi wa shule ya msingi Luvuyo nao hawakuwa mbali kumpongeza mh.mbunge kila mmoja alimchangia mbunge viazi viwili na yai moja moja kutambua mchango wake ktk shule hiyo ambayo watoto wake wamekabidhi msaada wa penzeli na rula na vifaa vya kichezo. Picha zitakujia hivi punde Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment