VYUO SABA VYA UTALII NJOMBE NA IRINGA VYA FUNGWA NA VETA.

MAMLAKA ya mafunzo ya  ufundi stadi Nchini (VETA) Nyanda za Juu kusini,  Imefunga vyuo saba vilivyopo katika mkoa wa Njombe na Iringa kwa kosa la kutokidhi vigezo ukiwemo usajili wa vyuo hivyo.
Ni kufuatia kufanya ziara ya kushitukiza iliyofanywa na Veta.
 Akiongea  na baadhi ya wamiliki na wanafunzi wa vyuo  mratibu wa Veta  nyanda za juu kusini Bw. john Mwanja amesema kuwa kutokana na wimbi la kuanzishwa kwa vyuo  ni vema wazazi wakaanza kufuatilia  usajili wa chuo ili kuepusha hasara ya muda pamoja na fedha pamoja na  vyeti wanavyopata  havitambuliwi na serikali hivyo inawawia vigumu kupata ajira.



 Prosper Mfugale ni Mwandishi wa Habari wa kituo cha Ebony Fm & Clouds Fm akiendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hilo.


 Majengo ya chuo cha Mosemi tawi la Njombe.
 Jengo la chuo cha Musoma Utalii kilichopo eneo la Mgendela Mjini Njombe.
 Moja ya darasa lililopo katika chuo hicho.
 Bw. john Mwanja akiwambia ukweli baadhi ya wanafunzi kuwa wamekuwa wakiibiwa fedha zao na kuwataka kuwaambia na wenzao wenye lengo la kujiunga na chuo.


 Hakuna aliyekuwa na Furaha mara baada kupokea kwa taarifa hiyo.
 Abrubakal Suleiman alisema kuwa yeye ni mkazi wa mjini Iringa alienda Mkoani Njombe Mara baada ya kuona tangazo ambalo halisadifu hali halisi iliyopo chuoni hapo.
 Hili ni jiko lililopo katika moja ya chuo ambacho inasemekana ilikuwa nyumba ya mtu
Mratibu wa vyuo hivyo akiendelea na ukaguzi katika chuo cha Eckross kilichopo sabasaba Mjini Njombe.
        
Akivitaja vyuo hivyo Vilivyofungiwa Mratibu huyo amesema kuwa ni Capricon Collage,Iringa Hotel and Tourism Collage vya Mjini Iringa, Chuo cha Mufindi Tourism Collage cha Mufindi, na Njombe ni Mosemi Collage, Musoma Utalii, Hokaido VTC  na Eckross Collage.

Katika hatua Nyingine aliwataka wazazi makini wanawapeleka watoto wao chuo cha kati kuwa kuangalia usajili wa vyuo hivyo na kuzitaja sifa ambazo za chuo kilichosajiliwa amesema kuwa ni pamoja na  Majengo  na vifaa vitakavyowasaidia wanafunzi kufanya kazi jambo ambalo limekuwa ni tatizo kwa vyuo vingi vilivyokosa sifa ya usajili.
 


Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment