ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
NA BARNABAS NJENJEMA,
LUDEWA ,NJOMBE
baadhi ya wakazi wilayani ludewa wakiwa katika shughuli za kilimo moja ya maeneo ya mjini licha ya kupigwa mafuku |
NA BARNABAS NJENJEMA,
LUDEWA ,NJOMBE
Baadhi
ya wananchi wilayani ludewa mkoani Njombe, wamelalamikia kitendo cha
serikali yao ya halmashauli wilaya ya ludewa , kutoa kauli ya kutolima karibu na makazi yao,
kwa kile walicho kiita kuwa hawana mashamba, na umri wao wengine ni
wazee hivyo hawawezi kulima mashamba ya mbali.
Wakizungumza
na njenje news blog,wananchi hao walisema kuwa, serikali ingetoa kauli
hiyo kwa kuwaangalia, kwa kuwa haijawatendea haki hasa wazee, ambao
hawanauwezo wakwenda umbali mrefu, kwa kuwa maisha yao ni magumu.
Hata
hivyo walisema kuwa ,kwa mda mrefu wamekuwa wakiishi kwa shida
kutokana na ugumu wa maisha ambao upo wilayani hapa hasa kwa wazee,
ambao wamesema hawana msaada wowote ule jambo ambalo wameomba
liangaliwe kwa ukaribu.
Aidhaa
wameiomba serikali yao kuwaangalia kwa karibu, kwa vile sasa ni
msimu wa kilimo, kwani kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yakitokea
msimu huu kipindi cha masika.
serikali ya halmashauli wilayani hapa ilitangaza kuwa ni marufuku kwa wananchi kulima karibu na makazi yao hasa mazao yanayokuwa marefu kama mahindi,mtama n.k
lengo la kutoa kauli hiyo ni kuepukana na baadhi ya maovu yanayotokea katika kioindi hiki cha masika ikiwa pamoja na ukabaji wa watu hasa nyakati za usiku pamoja na kuweka mazingira ya mjini kuwa safi muda wote..
0 comments:
Post a Comment