MBUNGE AWATUHUMU WENZIE KWA UBADHIRIFU

ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania




WABUNGE wamelipuliwa bungeni kuwa, baadhi yao ni wabadhirifu kutokana na kutumia fedha za umma kinyume cha sheria.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keisy (CCM), aliwalipua wenzake juzi, alipochangia mjadala kuhusu taarifa za kamati za Bunge za Hesabu za Serikali za Mitaa, Bajeti na Hesabu za Serikali Kuu.

Kutokana na hilo, Keisy ametaka sheria ichukue mkondo wake kwa kuwa waliofuja fedha hizo wanafahamika. Pia ametaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwakagua wabunge wanaotuhumiwa.

Licha ya kukataa kuwataja majina wabunge hao, Keisy alidai ana orodha yao.

Keisy alisema wabunge waliotafuna fedha za walipa kodi watatajwa na CAG, baada ya kuwakagua na kwamba, ikithibitika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria kwa kuwa ni wezi.
“Nashangaa badala ya kuchangia hoja mnaishambulia CCM na Serikali, kwani sisi hatujui maovu yenu? Naomba niweke wazi, kuna wabunge wamepewa fedha za safari kwenda kukagua miradi lakini hawakwenda, badala yake walibaki Dar es Salaam.

“Yuko mbunge mmoja mkubwa sana, alikatisha safari akaenda Dubai na mkewe, wako wengine wamepewa sh. milioni tano, sh. milioni sita ili kukagua miradi, badala ya kukaa siku nane wamekaa siku mbili wamerudi Dar es Salaam, kwani hatuwajui?” alihoji.

Mbunge huyo alisema hakuna sababu ya kuwanyooshea vidole mawaziri kwa kuwa wabunge nao ni mizigo kwa wananchi, kwa sababu wameshindwa kusimamia utendaji wao kuanzia katika halmashauri.

“Usitake kurusha mawe kwa mpinzani wako wakati unaishi kwenye nyumba ya vioo, hapa ndani mheshimiwa naibu spika kuna wabunge wezi, CAG atawataja baada ya kuwakagua,” alisema.
- See more at: http://onelovetz.blogspot.com/2013/12/mbunge-awatuhumu-wenzie-kwa-ubadhirifu.html#sthash.8RTXEUbx.xUCmOLq2.dpuf
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: