....IGP MWEMA AMTOA KAMANDA DIWANI ATHUMANI MBEYA

ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania

 IGP Mwema

MKUU wa Jeshi la Polisi,IGP Said Mwema amefanya

uteuzi wa makamanda wa Polisi kwa mikoa mitatu Mwanza,Mbeya

na Simiyu.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana na Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso ilisema IGP Mwma amemteua Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa

Polisi (SACP) Valentino Mlowola kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa

wa Mwanza.

Pia amemteua Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi

 (SACP)  Ahmed Msangi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Charles Mkumbo kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu.

Taarifa hiyo, ilisema  aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, SACP Salum Msangi amehamishiwa makao makuu ya Polisi Dar es Salaam.

IGP Mwema, amemhamisha Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara, Kamishina Msaidizi wa   Polisi (ACP) Jafary Ibrahim kwenda Kanda Maalum ya  Dar es Salaam  kuwa Mkuu wa Upelelezi.

Kwa uhamisho huo, nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Rogathe Mlasani kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es  Salaam.

Wengine waliohamishwa  ni Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) David  Mnyambuga kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam anakweenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina  Msaidizi wa Polisi (ACP) Martin Otieno kutoka Kanda Maalum ya Dar es salaam, amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi kuwa Mkuu wa kitengo cha Teknohama na Mrakibu wa Polisi (SP) Gidion  Msuya ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi  wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/ Rorya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tunduru OCD).
Na Mwandishi Wetu

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: