TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABari
ZIMBABWE KUTUA MCHANA KUIKABILI STARS
Kikosi cha Zimbabwe kinawasili leo
mchana (Novemba 18 mwaka huu) kuikabili Taifa Stars katika mechi ya
Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date
itakayofanyika kesho (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Msafara wa timu hiyo ukiwa na watu 30
utatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8
kamili mchana kwa ndege ya Kenya Airways yenye mruko namba KQ 484
kupitia Nairobi.
Kocha wa timu hiyo Ian Gorowa
atazungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu hiyo kutua JNIA.
Kiongozi wa msafara wa timu ya Zimbabwe ni John Phiri.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho ni
makipa; Frankson Busire, Maxwell Nyamupangedengu na Tapiwa Kapini.
Mabeki ni Carrington Nyadombo, Felix Chindungwe, Innocent Mapuranga,
Nkosana Siwela, Ocean Mushure na Patson Jaure.
Viungo ni Isaac Masami, Kundakwashe
Mahachi, Milton Neube, Misheck Mburayi, Obey Mwenehari na Silas Dylan
Songani. Washambuliaji ni Gerald Ndlovu, Lot Chiungwa, Nqobizitha
Masuku, Simba Sithole na Themba Ndlovu.
Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Uganda
wakati Kamishna atakuwa Leslie Liunda wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa
mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.
Viingilio ni sh. 5,000 kwa viti vya
rangi ya bluu na kijani, sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B, sh.
15,000 kwa VIP C wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000.
Tiketi zinauzwa kwenye magari maalumu
katika vituo vya; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers
uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Dar Live Mbagala, OilCom Ubungo, Uwanja
wa Uhuru, na kituo cha mafuta Buguruni
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment