SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limetangaza orodha ya wachezaji
46 ambao watachuana katika tuzo ya Mwanasoka Bora mwaka 2013 kupitia
hafla itakayofanyika Januari 9, mwakani, mjini Lagos, Nigeria.
Katika orodha hiyo, wachezaji 25 ni wanaocheza soka ya kulipwa nje ya bara hilo ambao watashindanishwa kivyao huku 21 wanaocheza soka katika klabu mbalimbali za ndani ya Afrika nao wakichuana.
Miongoni mwa nyota hao ambao kuingia kwao kwenye kapu hilo ni kutokana na mchango wao kwenye timu zao, ni Mbwana Samatta, nyota wa kimataifa wa Tanzania anayechezea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.
Samatta aliyeanzia soka yake katika timu ya vijana ya African Lyon ya Mbagala na baadaye Simba kabla ya kutwaliwa na TP Mazembe, atachuana na wakali wengine 20, akiwemo Mohammed Aboutreika aliyetwaa tuzo hiyo mara tatu.
Mara ya kwanza kwa Aboutreika kubeba tuzo hiyo iliyoanzishwa mwaka 2005, ni 2006, 2008 na 2012; hivyo yeye ameingia katika kapu hilo kuitetea tuzo ambayo kama atafanikiwa itaweka rekodi ya kuibeba mara nne.
Nyoya wengine katika mbio za tuzo hiyo, ni Adane Girma (St. George), Ahmed Fathi (Ahly), Alexis Yougouda Kada (Coton Sport), Ali Machani (CAB) na Bapidi Fils Jean Jules (Coton Sport).
Wengine ni Daine Marcelle-Klate (Orlando), Fakhreddine Ben Youssef (Tunisia) Getaneh Kebede (Bidvest Wits), Idrissa Kouyate (CS Sfaxien), Iheb Msakni (Esperance), Luyanda Lennox Bacela (Orlando) na Moez Ben Cherifia (Esperance).
Wamo pia Aboutrika (Ahly) na Rainford Kalaba (TP Mazembe), Senzo Meyiwa (Orlando) na Soumbeila Diakite (Stade Malien), Sunday Mba (Warri Wolves), Tresor Mputu (TP Mazembe), Waleed Soliman (Al Ahly) na Yannick N’djen (Esperance).
Hata hivyo, tukumbuke kuwa kati ya vigezo vya mshindi wa tuzo hiyo inayofanyika mara ya tisa tangu kuanzishwa kwake kwa lengo la kuongeza ushindani dimbani kwa nyota wanaocheza ndani ya Afrika, ni mchango wa mchezaji kwa klabu yake na timu ya taifa katika michuano ya kimataifa.
Nikitafakari hilo, naona wazi pamoja na mchango mkubwa wa Samatta kwa timu yake ya TP Mazembe iliyofanikiwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho ilikoangukia baada ya kufanya vibaya Ligi ya Mabingwa Afrika, kikwazo kimojawapo kwake kitakuwa kufanya vibaya kwa timu ya taifa, Taifa Stars.
Stars ikiwa pamoja na timu za Morocco, Ivory Coast na Gambia katika mbio za kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwakani nchini Brazil, iliishia hatua ya makundi baada ya kushika nafasi ya tatu.
Wakati nafasi ya kwanza ikishikwa na Ivory Coast ambayo juzi ilijitwalia tiketi ya Kombe la Dunia kwa kuwanfunga Senegal jumla ya mabao 4-2, nafasi ya pili ilishikwa na Morocco kisha Tanzania
na Gambia.
Kwa maneno mengine, japo mbio za Samatta katika tuzo hiyo zinaweza kukwazwa na rekodi mbaya ya Stars katika michuano hiyo ya kimataifa, bado mchezaji huyo anapaswa kupongezwa kwa mafanikio hayo na wengine wajifunze kutoka kwake.
Kutajwa kwenye orodha hiyo ya wakali 23, ni kutokana na mchango wake kwa klabu yake ya TP Mazembe iliyotinga fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuing’oa Stade Malien ya Mali kwa jumla ya 3-1.
Kwa ushindi huo, TP Mazembe sasa itakutana na CS Sfaxien ya Tunisia katika kuwania kitita cha dola 660,000 za Marekani ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Novemba 22 na 24 kabla
ya kurudiana kuamua bingwa.
Naamini, kwa vile mafanikio haya ya Samatta yametokana na mchango wake mkubwa katika mafanikio ya klabu yake, kwa namna yoyote ile wachezaji wa Tanzania waone haja ya kujifunza kutoka kwake kwani ameweza kuing’arisha Tanzania barani Afrika.
Unaweza usiyaone kamani mafanikio makubwa, lakini fikiria Afrika nzima kuna klabu ngapi na wachezaji wangapi, lakini Samatta akafanikiwa kuwemo kwenye orodha ya nyota bora 21 wa Afrika kwa sasa.
Kwa Tanzania, haya ni mwanzo wa mafanikio ya soka kwani hata nchi nyingine za Afrika zilizopiga hatua kubwa kisoka kama Ivory Coast, Ghana na nyinginezo zimefanya hivyo kutokana na mafanikio ya nyota mmoja mmoja wa nchi husika na mwishowe nchi nzima.
Namaliza kwa kusema hongera sana Samatta kuitangaza soka ya Tanzania kwa staili hiyo ya kuwemo kwenye orodha ya nyota bora 21 ya wanaowania tuzo hiyo kwani wengi wangetamani wachezaji wao wawemo, lakini haikuwezekana.
Hata kama safari hii hatashinda tuzo hiyo, naamini kama ataongeza juhudi zaidi dimbani, atajiweka kwenye mazingira ya kuendelea kuwemo kwenye mbio hizo, hivyo kuongeza uwezekano wa kushinda kulingana na vigezo vilivyowekwa na waratibu wa tuzo hiyo.

0 comments:
Post a Comment