MSAFARA WA WAZIRI WA UVUVI WAPATA AJALI SONGEA
Dereva wa Shirika la
Umeme TANESCO Tawi la Songea, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kusababisha
ajali katika Msafara wa Waziri wa Maendeleo Mifugo na Uvuvi Dr David
Mathayo.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi
wa Habari kuhusu Ajali ilyotokea kutoka Mbambabay – Songea na kusababisha watu
5 kujeruhiwa ambao walilazwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.
Akimtaja Dereva
anayeshikiliwa na Polisi amesema ni Ahamadi Hamisi 33 ambaye alikuwa akiendesha
Gari lenye lenye No. za Usajili SU 37788 TOYOTAHilax iliyo
igonga gari no stk 9906 mali ya RAS Mkoa wa Ruvuma Akiwataja
waandishi wa habari walio pata ajali na kulazwa ni Joseph
Mwambije, Lauf Mohamed, Cresensia Kapinga na Joicy Joliga
na mwingine ni Abiria mmoja aliyekuwa kwenye Gari la TANESCO.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki amesema Madereva wa Shirika la TANESCO
Mkoani Ruvuma pamoja na kupewa onyo wamekuwa wakiendelea kwanda kwa
mwendo kasi.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki amesema Madereva wa Shirika la TANESCO ambao
huendesha kwa kasi gari zao, mara nyingi wapitapo mitaani wamekuwa wakizomewa
na Wananchi ikiwa ni ishara ya kupinga mwendo mkali
lakini hata
hivyo wao huishia kuongeza mwendo . Dereva Ahamad Hamis anayeshikiliwa na
Polisi anahojiwa na upelelezi utakapokamilika atapelekwa Mahakamani.
Waziri wa Maendeleo,
uvuvi na Mifugo Dr. David Mathayo alikuwa Ziarani Mkoani Ruvuma kwa kutoa
Majibu ya Utafiti juu Samaki waliokuwa wanakufa Ovyo katika Ziwa Nyasa Wilayani
Nyasa na kugundua ilitokana na Uchafuzi wa Hali ya Hewa na siyo Sumu.
0 comments:
Post a Comment