JESCA MSAMBATAVANGU AONGOZA MAZISHI YA DIWANI FUTE , RAIS KIKWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI

                          Bw  Fute  enzi  wa  uhai  wake 
 

 Rais Kikwete Akitoa Salamu za Rambirambi Kwenye Msiba wa Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Lupyana Fute.

 Hapa ndio Nyumbani Kwa Marehemu Lupyana Fute Uzunguni Mjini Njombe Ambako Mwili wake Umeagwa Asubuhi ya Leo na Rais Kikwete Ametoa Heshima zake za Mwisho Hapo.







Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa  Jesca Msambatavangu akiongoza mazishi hayo kwa  kuweka shada la maua  leo
 Wakuu wa Wilaya za Njombe Kushoto Sarah Dumba,Katikati DC Wa Ileje na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi Wakiwa Wametoka Kuweka Shahada la Pamoja Kwenye Kaburi la Lupyana Fute.
 Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Njombe Wakimsikiza Mwenzao Lupyana Fute.
Kaburi Lake Likiwa Limewekwa Mashahada na Viongozi Mbalimbali Pamoja na Ndugu Jamaa na Marafiki wa Marehemu Lupyana Fute.

Na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapindunzi Mkoani Iringa  Bi. Jesca Msambatavangu Leo Amewaongoza Viongozi Mbalimbali wa Serikali , Chama ,  Dini Pamoja na Wananchi wa Wilaya za Njombe na Wanging'ombe Kwenye Mazishi ya Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Njombe Mjini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC Marehemu Lupyana Godfrey Fute.

Akiongea Wakati wa Kuongoza Mazishi Hayo Kwaniaba ya CCM Taifa Bi. Msambatavangu Amesema Chama cha Mapinduzi Kimepoteza Mtu Makini na Mchapakazi na Kusema Kuwa CCM Iko Pamoja na Familia ya Marehemu
Katika Kipindi Hiki cha

Majonzi.
 

Akitoa Salamu za Serikali Kwaniaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete , Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge Ameiomba Familia ya Marehemu  Kutoanzisha Mafarakano Kufuatia Kifo Chake.

Kwa Upande Wake Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Njombe Askofu Japhet Isaya Mengele Amewataka Wanasiasa Kutumia Harakati Zao na Ushirikiano Wao Katika Kuyaenzi Yale Yote Yaliyo Mema Pamoja na Aliyoyaacha Marehemu Lupyana Fute.

Akisoma Histori ya Marehemu Lupyana Fute , Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Hosea Mpagike Amesema Kuwa Marehemu Alifariki Kwa Shinikizo la Damu Oktoba 19 Mwaka Huu na Kwamba  Marehedmu Amewaacha Watoto Wanne na Mjane Mmoja.

Marehemu Lupyana Fute Amefariki  Juzi Jioni Majira ya Saa Kumi na Moja na Nusu Jioni Baada ya Kuzuka Kwa Moto Katika Chumba cha Kuhifadhia Vifaa Kwenye Jengo la Ofisi Yake Iliyopo Karibu na Zahanati ya Tumaini  Mjini Njombe Licha ya Moto Huo  Kufanikiwa Kuzimwa.

Mungu Alitoa na Mungu Ametwaa  Jina la Bwana Lihimidiwe
Mungu  Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi Amini.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: