Serikali imewaagiza polisi mkoani Mbeya kumsaka mahali popote alipo
aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Nazarene iliyopo jijini hapa(jina
tunalo) kwa madai ya kufanya udanganyifu wakati wa Mitihani ya Taifa ya
Kidato cha pili akiwashirikisha wanafunzi sita wa kidato cha tatu Oktoba
7 mwaka huu.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo alitoa
agizo hilo jana alipotembelea shule hiyo kujua ukweli, ambapo pia
aliagiza wanafunzi sita wa kidato cha tatu walioshirikiana na mwalimu
huyo kusimamishwa masomo kwa kipindi kisichojulikana ili kupisha
uchunguzi.
Ilielezwa kwamba wanafunzi hao walikamatwa wakifanya mitihani ya
kidato cha pili kwa kutumia majina bandia ambayo walidai walipewa na
mkuu wao wa shule na wala hayakuwa ya wanafunzi wa shule hiyo.
Baada ya wasimamizi wa mitihani kuwakamata wanafunzi hao, ilielezwa
kwamba mkuu wa shule hiyo ambayo inamilikiwa na Kanisa la Nazarene la
Kenya alitoweka na hadi sasa hajulikani aliko.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment